Breaking News

DOYO ATOA ANGALIZO KWA TAMISEMI NA WANASIASA KUELEKEA UCHAGUZI

Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo ameiomba serikali kupitia TAMISEMI kuongeza mda wa ratiba za uchaguzi huo pamoja na wanasiasa kuacha kufanya siasa ambazo zinadhalilisha na kuchafua watu na utu wao.

Akizungumza katika Uzinduzi wa KAMPENI mpya ya chama hicho kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, “Fyeka CCM” uliofanyika katika ofisi za Makao makuu ya chama hicho zilizopo Tandika Jijini Dar Es Salaam

Alisema chama kimekuwa kikifatilia mijadala na matamko mbalimbali hususani yanayotolewa na baadhi ya wanasiasa kutoa kwa kutumia lugha zisizokuwa nzuri kwa viongozi wa Serikali akiweno Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kauli na tuhuma hizo mara nyingi zimekuwa zikitolewa kwa lugha ziziso na staha na maadili niviombe vyombo vya usalama kuchukua hatua stahiki kwa lengo la kukomesha Tabia hii mbaya ambayo imekuwa ikishamili siku za hivi karibuni.

"Napenda kutoa Rai kwa vyombo vya usalama kuchukua hatua kwa wale wote wanatoa kauli za kudhalilisha viongozi ili kuepusha kuendelea kukuwa kwa vitendo hivi ambavyo vimekuwa vikishika kasi siku za hivi karibuni" Alisema Doyo.

Alisema chama Cha NLD kimejipanga kufanya siasa safi na za kujenga hoja nitoe wito kwa Viongozi wote katika ngazi mbambali ndani ya chama na wanachama kutotoa maneno ya kashfa na kutweza utu wa mtu na waheshimu Mamlaka kwa kuwa na Uhuru wenye mipaka.

“Katika itikadi ya chama chetu tunaamini kuwepo Kwa Uhuru ila wenye mipaka na wa kujenga hoja juu ya namna gani wanaweza kuwasaidia watanzania kutatua changamoto zao na si kutukana diwani,mbunge au Rais wa nchi hivyo nawasihi wanachama wa NLD mkaawaambie watanzania namna mtakavyowakwamua na kujenga hoja za maendeleo, mtapata wanachama bila kutukana viongozi kwani nao wana watoto” Alisema Bw. Doyo 

Akizungumza mipango ya chama kuelekea uchaguzi wa Vijiji na Mitaa na ule wa wabunge na urais 2025 amesema kupitia Oparesheni fyeka CCM tutasimamisha wagombea watakaoleta ushindani na kushinda Kwa kishindo uchaguzi huo.

Katika hatua nyingine katibu huyo amelalamikia kalenda (ratiba) ya uchaguzi wa serikali za mitaa iliyoyolewa na TAMISEMI na kudai imewabana na haitoi muda wa kutosha Kwa vyama kujiandaa na kujipanga vyema.

“Tamisemi isipime vyama vyetu kwamba vinaweza kushindana na chama tawala Kwa kufanya kampeni muda siku Saba pekee,hivyo tunaomba ratiba iongezwe muda ili tuweze kumudu hali ya uchaguzi kwani Kwa namna vyama vyetu hali zake zilivyo inaleta shida na hatusemi uchaguzi uhairishwe huo siyo msimamo wetu tunaomba tu ziongezwe siku ili tujipange vyema”,amesema.

Amesema chama hicho kitasimamisha wagombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na tayari timu yake iko Mikoani kuhakikisha wagombea wanapatikana.

Naye katibu Mkuu mstaafu wa NLD Tozy Matwanga amesema kuwa ili kujenga serikali ni lazima chama kiingie katika uchaguzi,hivyo na wao Kama chama watashiriki chaguzi zote na hawatogomea.

Hata hivyo chama hicho kimewapokea wanachama wapya kutoka chama cha ACT Wazalendo na ADC akiwemo Bi Mariam Ahmed Sijaona ambaye alikuwa mjumbe wa halmashauri kuu ngome ya wanawake Taifa ya ACT ambaye amesema amechukua maamuzi ya kukikacha na kujiunga na NLD baada ya kusoma na kuridhishwa na Sera zake.

No comments