Breaking News

CHAMA CHA NLD CHAZINDUA OPERESHENI "FYEKA CCM"

Chama cha National League for Democracy (NLD) kimezindua operesheni fyeka CCM 2024/2025 yenye lengo la kuki ndoa Chama Chama cha Mapinduzi (CCM) madarakani iki kishike Dola.

Akizungumza makao makuu ya chama hicho Septemba 29, 2024 jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa NLD Doyo Hassan Doyo amesema operesheni hiyo itafanyika kwa viongizi kufanya ziara katika mikoa mbalimbali nchini ambapo awamu ya kwanza itafanyika katika mikoa 10.

Kwamba wiki ijayo baadhi ya viongozi watakuwa katika Mkoa wa Tanga, wengine watakuwa mikoa ya Lindi na Mtwara, Ruvuma, Mwanza, Mara na Kagera.

"Hivyo tunazindua leo hapa kampeni hii na tunakwenda kutengeneza wagimbea watakaoleta ushindi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani," amesema Doyo.

Hata hivyo akizungumzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa ameomba Wizara ya Tamisemi kuongeza muda kwani ni mchache Kwa vyama kujiandaa na michakato hiyo katika kuandaa wagombea na kampeni.

Kadhalika ameomba kanuni ya Uchaguzi huo iwekwe wazi ili waweze kuijua na kuandaa wagombea waliosahihi kwani Hadi sasa kanuni haijuilikani na hivyo kuwa kikwazo kwao kuelekea uchaguzi huo.

Hata hivyo Doyo amesema Chama hicho kimepanga kusimamisha wagombea Nchi nzima katika uchaguzi huo ambapo ameahidi kuwa watafanya siasa za Maendeleo na za kistaarabu bila kutukana wagombea wengine.

No comments