Breaking News

UZINDUZI WA KAMPENI YA "TUNAZIMA ZOTE TUNAWASHA YA KIJANI" WAISIMAMISHA DAR

Mjumbe wa NEC, Idara ya Organization wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Issa Gavu amewataka vijana kujitokeza Kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kushiriki kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi za Serikali za Mitaa na Vitongoji utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Wito huo huo ameutoa leo, Julai 6, 2024 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam wakati, akizungumza na vijana mbalimbali wa jijini humo wakati akizindua kampeni kwa vijana kutumia fursa zilizopo ambazo zimetengenezwa na Serikali ya Sita ili kujikwamua kiuchumi.

"Nawaomba vijana ambao mmejitokeza hapa kwa wingi kwa hakika mmetuheshimisha na wale mnaotusikiliza na kutuangalia  kupitia mitandao ya kijamii mjitokeze  kugombea kushiriki kikamilifu kwenye siasa na kuwania  nafasi mbalimbali za uongozi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kulijenga taifa imara lenye viongozi bora.
"Leo tunazindua Kampeni ya Tunazima Zoote, Tutawasha Kijani kupitia Umoja wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM ) lengo ni kuhamasisha vijana kujiandaa na uchaguzi na mjiandikishe kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura hivyo nawaomba tuwe wamoja kupitia UVCCM ili tufanikiwe pamoja na kuipeperusha vema bendera ya CCM, kwani nyingi ndio ngumu muhimu katika uhai wa chama  chetu," amesema

Gavu ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha, Katibu Mkuu wa chama hicho, Mwanadiplomasia Dk. Emmanuel  Nchimbi , amesema chama hicho kinawapa fursa vijana ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi Kwa maana, Tanzania ya leo na ya kesho inaundwa na vijana na  endapo watatumia vizuri nafasi watakazozipata ni vizuri  kuendeleza amani, imoja na mshikamano uliopo nchini.

Amesisitiza kuwa  Serikali iliopo madarakani chini ya Usimamizi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassani imewapa  vijana fursa mbalimbali ikiwemo, mikopo itakayowawezsha kujikwamua kiuchumi.
Pia kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohamed Kawaida amewataka vijana kuhakikisha mikoa yote inazimwa na kuwasha rangi ya kijani ili kuunga mkono juhudi mbalimbali anazozifanya Rais Samia katika kulijenga Taifa.

Naye Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Jokate Mwegelo amesema wamejipanga kuhakikisha,  uchaguzi wa  Serikali za Mitaa na vitongoji,  pamoja na uchaguzi Mkuu, utakaofanyika Oktoba mwakanj unaleta mafanikio na chama kinashinda kwa kishindo.

"Chama kinajua kwamba vijana ndio msingi wa mafanikio katika taifa ndio maana Serikali ya Awamu ya Sita, imekuwa ikitoa fursa mbalimbali kwa kundi hili, kinachotakiwa ni kuendeleza mshikamano wetu nchi nzima na kufanikisha ushindi wa kishindo katika chaguzi zilizombele yetu," amesema. 

Pia amesisitiza vijana kuendelea kuilinda tunu ya amani ambayo imelindwa kwa nguvu kubwa na viongozi kwa maslahi ya watanzania wote bila kujali itikadi mbalimbali.










No comments