Breaking News

BRELA KUANZA KUTUMIA MIFUMO MIPYA YA USAJILI JUNE 24, 2024

Wakala wa Usajili wa Leseni za Biashara (BRELA), wamesema kuwa kuanzia Jumatatu, Juni 24, 2024 wanatarajia kuanza kutumia mifumo miwili mipya ya kimtandao katika shughuli zake mbalimbali ikiwemo ya usajili.

Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu kutoka BRELA, Bi Loy Mhando amebainisha hayo mkoani Morogoro wakati akiwasilisha mada katika semina kwa Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu kuwa mifumo hiyo maarufu ya ‘Oline Registration System na Tanzania Business Portal"

Alisema Online Registration System ndio itakayotumika kusajili kampuni na Majina ya Biashara, leseni za viwanda pia ndio mfumo unaotumika kwa alama za biashara na huduma pamoja na Hataza, hivyo kwa anayehitaji kulinda alama yake atawasilisha maombi kupitia mfumo huo wa usajili kwa njia ya mtandao (ORS).

“Muombaji anapoomba lazima awasilishe anataka ulinzi katika daraja lipi, kuna daraja la Alama za Biashara na Huduma ambazo zipo 45 na zimewekwa makundi kulingana na bidhaa zinazofanana, mfano ukitaka kusajili maji utasema daraja 32 ambazo zinahusiana na maji na vinywaji laini". Alisema Bi. Mhando.

Alisema kuanzia daraja 1 hadi 34 zinahusika na bidhaa, daraja 35 hadi 45 zinahusika na huduma kwa hiyo maombi yanapowasilishwa kama ni Mtanzania awe na namba ya Nida, raia wa kigeni hawezi kuomba moja kwa moja bali ni lazima atumie wakala wa ndani.

Alisema mwombaji anaweza kuwa mtu binafasi au kampuni na kusisitiza kuwa jina la biashara haliwezi kuomba ulinzi wa alama za biashara na huduma kwa sababu haina utu kisheria, Kampuni ina utu kisheria hivyo inaweza kuomba alama ya biashara na huduma.

Aidha Bi. Mhando alimeongeza kuwa ada za usajili wa alama zipo katika makundi tofauti na hazilipwi kwa wakati mmoja huku akibainisha kuwa ada ya maombi ni shilingi 50, 000, pia kabla ya ada ni lazima kutangazwa na hii ni takwa la kisheria kabla haujasaliwa lazima itangazwe ili kutoa nafasi kwa wenye mapingamizi.

No comments