MAENDELEO BENKI YATAPA FAIDA YA BILLION 2.3 MWAKA 2023

Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Benki ya Maendeleo Pls, Dkt. Ibrahim Mwangalaba akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao Makuu ya Bank hiyo Jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Mbatilo.

Dar es Salaam 
Maendeleo Bank Plc kwa mwaka 2023 imetangaza kupata faida kwa asilimia 66 baada ya kodi ambapo mapato yameonesha kukua na kuongezeka hadi shilingi Bilioni 2.3 kutoka shilingi Bilioni 1.4 mwaka 2022 ikichangiwa na jitihada za serikali kuweka mazingira bora na uimarishwaji wa uchumi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam wakati Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Dkt. Ibrahim Mwangalaba amesema pamoja na benki hiyo kuandika historia ya kupata faida kwa miaka tisa mfululizo mafanikio hayo yamechangiwa zaidi na mikakati mizuri ambayo benki ilijiwekea kwa mwaka 2023 pamoja na usimamizi bora wa watendaji wake.

"Mafanikio Makubwa ambayo yanaendelea kuonekana ni ushirikiano kati ya wafanyakazi, bodi ya wakurugenzi, wateja na wadau mbalimbali pamoja na mikakati mizuri iliyojiwekwa benki hiyo kwa mwaka 2023" Alisema Dkt. Mwangalaba.

Alisema moja ya vichocheo vya mafanikio ya Benki hiyo ya kwanza nchini kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE,)ni pamoja na kuimarika kwa ubora wa mikopo kutoka mikopo chechefu ya asilimia 5.2 mwaka 2022 hadi kufikia asilimia 4.95 mwaka 2023 kutokana na kuimarika kwa hali uchumi na hivyo wateja kulipa mikopo kwa wakati.

Ametaja nyingine kuwa ni kuongezeko Amana za wateja kwa asilimia 15 kutoka shilingi Bilioni 78.0 mwaka 2022 hadi kufikia shilingi Bilioni 90.0 kwa mwaka 2023.

“Mikopo kwa wateja imeongezeka kwa asilimia 21 kutoka shilingi Bilioni 61.0 hadi shilingi Bilioni 74.0 kwa mwaka 2023 ambapo ukuaji huu utaendelea kutokana na Benki kiwa imejipanga kutoa huduma kwa ufanisi zaidi kwa wateja wake” Alisema Dkt. Mwangalaba.

Akizungumzia mtaji na mikakati ya benki hiyo kuwafikia wananchi katika mikoa yote nchini amesema, Benki tayali imefikisha mtaji wa Shilingi Bilioni 19 ambao unakidhi benki kufanya kazi nchini nzima na tayari wameanza mazungumzo na wasimamizi wao ambao ni Benki Kuu ya Tanzania (BOT,) kupata kibali cha kufungua matawi mikoani yote mwaka huu.

Alisema Utendaji kazi bora wa mwaka 2023 umejenga msingi thabiti wa utendaji kwa mwaka 2024 ambapo wamejipanga kutanua huduma zaidi kwa kufungua angalau tawi moja na mawakala wapya zaidi ya 500 kutokana na mafanikio makubwa ya mwaka 2023 ambapo walifunga na mawakala 1600 katika mikoa 11 ambao walikusanya zaidi ya Bilioni 5 kila mwezi kama amana kupitia wateja.

“Benki tayali imeshajikita zaidi katika kuwekeza katika teknolojia ambapo kwa mwaka 2024 imejipanga kuanzisha huduma mpya za kidigitali ikiwemo Benki mtandao yaani Internet Banking, mfumo wa ukusanyaji malipo ikiwemo ada za shule (PCS,) na mikopo kwa njia ya simu ambayo itawezesha benki kuongeza faida kwa fedha za wanahisa kwa mwaka 2024 na kuboresha njia mbadala za upatikanaji wa huduma za wateja

Katika hatua nyingne Dkt. Mwangalaba amezunguzmia hatua ambazo benki hiyo imwluwa ikizichukua kuhakikisha inasogeza huduma zake karibu kwa jamii amesema tayali benki hiyo imefungua tawi jipya Mbagala jijini Dar es Salaam likiwa tawi la tano.

No comments