DKT MWINYI MGENI RASMI UZINDUZI WA CHUO KIKUU CHA TUMAINI (DarTU)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kupandishwa hadhi kwa Chuo kikuu cha Tumaini Dar es salaam (DarTU) uzinduzi utakaofanyika tarehe 19 April 2024 jijini Dar es salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam makamu Mwenyekiti wa chuo hicho, Profesa Burton Mwamila amesema January mosi, 2024 tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) kukipandisha hadhi chuo kikuu kishiriki cha Tumaini Dar es salaam (TUDARCo) na Tumaini Makumira kilichopo Arusha kuwa rasmi chuo kikuu.
"Kufatia kupandishwa hadhi na TCU kuwa chuo kikuu na kupewa cheti cha Ithibati ikiwa ni pamoja na kutangazwa katika gazeti la serikali toleo na 11 la march 15, 2024 sasa kimezaliwa rasmi kwa chuo kikuu cha Tumaini (DarTU)". Alisema Prof. Mwamila.
Alisema uzinduzi utatanguliwa na ibada maalum ya shukrani itaongozwana askofu Jackson Sosthenes kutoka kanisa la Aglikani Tarehe 18 mwezi huu ibada ambayo itaudhuriwa na viongozi kutoka Dayosisi ya mashariki na pwani ikiwakilishwa na Baba Askofu, Msaidizi wa Askofu, Wakuu wa Majimbo yote Sita, Wachungaji wa Shirika, Wainjilisti, Washirika wa kila Ushirika wa DMP pamoja na Vijana kutoka matawi yote 20.
Aidha Profesa Mwamila aliongeza kuwa uzinduzi huo pia utaenda sambamba na uzinduzi wa mfuko wa ufadhili kwa wanafunzi wasio na uwezo waliokatisha masomo kwa kukosa ada (students scholarship Endowment Fund - SSEF) pamoja na uzinduzi wa Atamizi ya Biashara na Teknolojia kwa ajili ya kulea, kuchochea na kuendeleza ubunifu wa wajasiliamali unaobiasharisha maarifa na ujuzi wanaopewa darasani kwa lengo la kuzalisha ajira na kujiajili kirahisi.
Alisema chuo kimekuwa kikijipambanua kwa kuhimiza, kusimamia na kuendeleza "Maadili mema, Mawazo ya kujenga na mtizamo chanya" kwa lengo la kuhakikisha kuwa ujifinzaji bora kwa wanafunzi wake na uraia wema kwa umma na taifa.
Chuo cha Tumaini (DarTU) kina takribani wanafunzi 4500 wanaosomea program ngazi za astashahada mpaka shahada za uzamili katika fani mbalimbali katika skuli zake tano ikiwemo Biashara, Elimu na makuzi ya binadamu, Teknolojia za kidijitari, Insia, Sayansi ya jamii, Sheria na Haki.
Post Comment
No comments