Breaking News

DCPC NA JESHI LA POLISI KUSHIRIKIANA KIMKAKATI KUDUMISHA USALAMA WA WAANDISHI

Picha ya pamoja wajumbe wa kamati mpya iliyoundwa kwa ajili ya kujenga ushirikiano wa kimkakati kati ya jeshi la polisi na Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC).
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, kamishna Msaidizi wa polisi (SACP) Muliro Muliro akizungumza katika mdahalo kati ya DCPC na Polisi kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari wawapo kazini pamoja na suala zima la kusimamia haki na sheria. 
Askofu Emaus Mwamakula wa Kanisa la Uamsho la Morovian akichangia mada katika mdahalo kati ya DCPC na Polisi kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari wawapo kazini pamoja na suala zima la kusimamia haki na sheria
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC), Sam Kamalamo akizungumza katika mdahalo kati ya DCPC na Polisi kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari wawapo kazini pamoja na suala zima la kusimamia haki na sheria.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), John Malulu, ambaye pia ni RPC wa Mkoa wa Kipolisi Temeke akiwasilisha mada katika mdahalo kati ya DCPC na Polisi kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari wawapo kazini pamoja na suala zima la kusimamia haki na sheria.
Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC), akichangia mada katika mdahalo kati ya DCPC na Polisi kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari wawapo kazini pamoja na suala zima la kusimamia haki na sheria.

Dar es Salaam
Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC) na Jeshi la Polisi Kanda Maalum (Dar es Salaam), wamefungua ukurasa mpya wa ushirikiano kimkakati kwa kuunda kamati ndogo itakayosimamia na kufuatilia ulinzi na usalama wa waandishi wa habari wanapokuwa kazini

Kamati hiyo ambayo itakuwa na wajumbe sita imeundwa Machi 22, mara baada ya mdahalo wa majumuisho kati ya DCPC na Jeshi la Polisi. 

Wajumbe wa wataounda Kamati hiyo ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), John Malulu, ambaye pia ni RPC wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Askofu Emaus Mwamakula na Sheikh wa Wilaya ya Ilala, Adam Mwinyipingu.

Wengine ni Wakili Mkumbo Emmanuel, Fatma Jalala Katibu Mkuu wa DCPC na Bakari Kimwanga ambaye ni (mwanachama wa DCPC).

Kuundwa kwa Kamati hiyo ni matokeo ya midahalo mitatu kati ya DCPC na Polisi kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari wawapo kazini pamoja na suala zima la kusimamia haki na sheria. 

Akizungumza katika mdahalo huo Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, kamishna Msaidizi wa polisi (SACP) Muliro Muliro ameahidi kuwa jeshi la polisi litaendelea kusimamia haki na sheria kama vile zinavyotambuliwa kitaifa na kimataifa na kwamba anawahakikishia waandishi wa habari kuwa salama.

Mdahalo huo ambao uliratibiwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) chini ya udhaminiwa na shirika la IMS, ilihusisha Kanda Maalum (Ilala ikiwemo), Temeke na Kinondoni, ambapo maazimio kadhaa ya kiutendaji yalifikiwa ulianza Novemba 2023 na kumalizika Februari 2024,

Miongoni ya maazimio hayo ni pamoja na kuwepo na mabonanza ya kimichezo kwa lengo la kujenga ukaribu, kuhakikisha usalama wa waandishi kazi pamoja na katika operesheni za polisi, kuwepo kwa kanzidata ya waandishi wa habari ambayo itatambuliwa na polisi, sambamba na jeshi la Polisi kufanya kazi kushirikia na DCPC.
Baadhi ya washiriki kutoka jeshi la polisi wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mdahalo kati ya DCPC na Polisi kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari wawapo kazini pamoja na suala zima la kusimamia haki na sheria

Baadhi y washiriki kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC), wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mdahalo kati ya DCPC na Polisi kuhusu ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari wawapo kazini pamoja na suala zima la kusimamia haki na sheria.