Breaking News

TANZANIA YAPAA HUDUMA ZA MAWASILIANO, LINE ZAIDI YA 70 ZASAJILIWA

Tanzania imetajwa kuwa moja ya nchi yenye maendeleo makubwa ya huduma za mawasiliano kwa gharama nafuu mijini na vijijini kwa kufanikisha laini za simu milioni 72.5 mpaka mwezi machi 2024 kutoka laini milioni 64.1 Juni mwaka 2023.

Imefahamika pia kuwa Katika kipindi hicho idadi ya watumiaji wa huduma za mitandao ya intaneti imekua hadi kufikia watu milioni 36.8

Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wasichana na Tehama.

“Idadi kubwa ya Watanzania wa mijini na vijijini imefikiwa na huduma ya mawasiliano ya simu na mitandao ya Internet, haya ni maendeleo makubwa katika sekta ya mawasiliano hapa nchini,”. Alisema Bi. Mahundi

Alisema idadi hiyo ni kubwa kufikiwa katika utoaji wa huduma hizo, ukilinganisha na nchi zingine huku upatikanaji wa huduma kumeiwezesha jamii ya watanzania kushiriki ipasavyo uchumi wa kidijiti.

Aidha Naibu waziri ameviagiza Vyuo Vikuu, Vyuo vya katiz shule za sekondari na Msingi kuanzisha klabu za kidijiti ili kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi na kukuza ujuzi wa kidijiti.

“Tutoe kipaumbele zaidi kwa watoto wa kike ili wapende kusoma masomo ya sayansi ili wasiwe wababaishaji na mambo yao yataenda vizuri lakini pia utumiaji wa Tehama utawezesha kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa". Alisema Bi. Mahundi. 

Source; Ngalisho News