Breaking News

TAKUKURU KINONDONI YAPOKEA MALALAMIKO 84 KATIKA KIPINDI CHA MIEZI MITATU

Na Magrethy Katengu, 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), wilaya ya Kinondoni imesema katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi ,2024 wamefanikiwa kupokea jumla ya malalamiko 84 ambapo yaliyohusu rushwa ni 40 yasiyohusu rushwa ni 44.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Naibu Mkuu Takukuru (M) Kinondoni, Elizabeth Mokiwa amesema malalamiko ambayo hayahusu rushwa walalamikaji wengine wameshauriwa na mjadala kufungwa huku wengine wameelekezwa sehemu sahihi ya kupeleka malalamiko yao yanayohusu rushwa majalada yanaendelea kushughulikiwa katika hatua mbalimbali.

”Mchanganuo malalamiko tuliyoletewa ni Asasi binafsi 35 , TAMISEMI/ Manispaa19, Mahakama 6, Polisi 7, Benki 5, Elimu 3, Wizara ya Ardhi 2, TLB 1, Dini 1, JKT 1, NIDA 1, TRA 2, DAWASA 1 pia katika kipindi husika mashauri mawili 2 yametolewa maamuzi na Jamuhuri imeshinda na tumefungua mashauri mapya matatu 3 huku mashauri 19 yanaendelea mahakamani “. Alisema Bi. Elizabeth.

Alisema TAKUKURU Kinondoni inaendelea kufuatia miradi 6 yenye thamani zaidi ya shilingi Bilion 61 na kubaini mapungufu machache ambayo wahusika wameshauriwa kurekebisha na tunaendelea kufuatia hadi miradi itakapokamilika.

“Tutaendelea kutoa elimu ya rushwa na dawa za kulevya kwa vijana walioko mashuleni kupitia Vipindi vya Tv, Redio na Magazeti pia warsha mbambali ili watambue madhara ya rushwa na dawa za kulevya na kuchukua hafua kwa maslahi ya Taifa”. Alisema Bi. Elizabeth.

Aidha Bi. Elizabeth aliongeza kuwa Tunatoa wito kwa wananchi wa Kinondoni kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU na wanapopata taarifa zozote za rushwa watoe taarifa kwa kupiga au ujumbe mfupi kwenda namba ya dharura 113 ni bure.