Breaking News

WAZIRI SILAA AWATAKA WASAJILI HATI KUACHA URASIMU NA LUGHA CHAFU

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amewataka Wasajili wa Hati wa Ofisi za Kamishna wa Ardhi Dar es salaam na Pwani kuacha urasimu kabla hajaanza kuwachukulia hatua kali za kinidhamu.

Waziri Silaa ametoa kauli hiyo wakati alipofanya kikao maalumu na wasajili hao katika Ofisi yake iliyopo jijini Dar es salaa na kuwapa siku mbili tu za kujibadilisha kwa kutoa miamala ya hati haraka na kwa wakati bila urasimu.

Amesema watumishi hao wamekithiri kwa lugha chafu na zisizo ridhisha kwa wananchi wanaotaka huduma katika ofisi hiyo ambayo ndio inahusika na kuandaa na kutoa hatimiliki za ardhi pamoja na miamala mingine ya kisheria kwa wananchi.

Aidha, amesema hatomuamisha mtu kwa uzembe na badala yake atawachukulia hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha kazi watakao bainika na maelekezo hayo ameishampa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

No comments