DIWANI TIAMAS AELEZEA MABORESHO MAKUBWA YALIYOFANYIKA MSOMERA
Diwani wa Kata ya Kakesio Msomera mkoani Tanga, bwana Johannes Tiamas akizungumza na waandishi wa habari juu ya zoezi la kuwahamisha kwa hiari wananchi kutoka Ngorongoro kuja Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga
Msomera - Tanga
Diwani wa Kata ya Kakesio msomera mkoani Tanga, bwana Johannes Tiamas amewataka wananchi ambao bado awajahama kwa hiari kutoka Ngorongoro kuja Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga kufanya maamuzi ya kuhamia kwani kuna mabadiliko makubwa ikilinganishwa na mwanzo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kujionea makazi hayo mapya ya waliokuwa wananchi wa Ngorongoro mkoani Tanga amesema maisha ya wananchi wa Ngorongoro waliohamia kwa hiari katika maeneo ya hayo ni tofauti ikilinganishwa na mwanzo.
“Kuna mabadiliko makubwa kwa watu wa Ngorongoro ikiwemo watu wameanza kulima na kuanza kufaidi na kuwa njia mbadala ya kutegemea mifugo kuna mabadiliko ya mavazi" Alisema Diwani Tiamas.
Alisema kumekuwepo na maboresho makubwa sana ambapo wananchi wa ngorongoro kwa sasa wameanza kujenga, kuna umeme pamoja na kuwa na uhuru tofauti na kule Ngorongoro.
“Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuongeza wingo kwa wakazi wanaotaka kuhama kwa hiari kutoka eneo la ngorongoro na hawataki kuhamia msomera kuchagua sehemu nyingine kwa upande wangu mimi nawakaribisha hapa na wasiwe na hofu yoyote” Alisema Diwani Tiamas.
Nae mwakilishi wa waliokuwa wakazi wa Ngorongoro Mingati Molel amepongeza jitihada na hatua zinazochukuliwa na serikali ikiwemo kutoa elimu kwa wakazi hao hili waweze kuhama kwa hiari
“Kwanza naishukuru sana serikali kwani wametutendea mema, mimi umri wangu wa miaka 68 watoto wangu hawajawai kushiba chakula kilichotokana na mkono wangu, lakini sahivi wanashiba” Alisema Molel.
Picha mbalimbali za baadhi ya wananchi waliokubali kuhama kwa hiari kutoka Ngorongoro kuja Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga
Post Comment
No comments