NCAA HAKUNA UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU ZOEZI LA UHAMISHAJI NGORONGORO.
Kamishna msaidizi wa uhifadhi, Mipango ufuatiliaji na Tathmini kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Bi. Lilian Magoma akiongea na waandishi wa habari katika ziara ya kujionea zoezi la kuwahamisha wananchi wa Ngorongoro kwa hiari na kuwapeleka katika maeneo yaliyotengwa likiwemo la Msomera Wilayani Handeni mkoani Tanga
Afisa Uhifadhi Mwandamizi kutoka NCAA, bwana Kassim Nyaki akifafanua jambo wakati akiongea na waandishi wa habari katika ziara ya kujionea zoezi la kuwahamisha wananchi wa Ngorongoro kwa hiari na kuwapeleka katika maeneo yaliyotengwa likiwemo la Msomera Wilayani Handeni mkoani Tanga.
Ngorongoro:
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesisitiza kuwa hakuna ukiukwaji wa haki za binadamu katika zoezi la kuwahamisha wananchi wa Ngorongoro kwa hiari na kuwapeleka katika maeneo yaliyotengwa likiwemo la Msomera Wilayani Handeni mkoani Tanga
Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya kujionea zoezi la kuwahamisha wananchi wa Ngorongoro kwa hiari na kuwapeleka katika maeneo yaliyotengwa likiwemo la Msomera Wilayani Handeni mkoani Tanga Kamishna msaidizi wa uhifadhi, Mipango ufuatiliaji na Tathmini kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Bi. Lilian Magoma amesema hakuna ukiukwaji wa haki za binadamu katika zoezi la kuwahamisha wananchi hao wa Ngorongoro
“kumekuwepo na baadhi ya watu (wanaharakati) toka ndani na nje ya nchi wakitumia vyombo vya habari kusema kunaukiukwaji wa haki za binadamu jambo ambalo sio kweli kwani utelekezaji wa zoezi hili umezingatia sheria na utu katika kuwahamisha” Alisema Bi. Magoma.
Alisema serikali imeingia Gharama kubwa ikiwemo kuwalipa fidia, kuwasafirishia mali zao na kutoa motisha ya milioni kumi ambayo ametoa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani.
Alisema serikali imekuwa inatoa wito kwa wananchi wa Ngorongoro kuhama kwa hiari sehemu hiyo kwani kuna faida kubwa ikiwemo kulinda Hifadhi hiyo.
Kwa Upande wake Afisa Uhifadhi Mwandamizi kutoka NCAA, Kassim Nyaki,amesema katika katika awamu hii ya pili iliyoanza mwaka jana lengo ni kujenga nyumba 5000 katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wananchi wa Ngorongoro ikiwemo eneo la Msomela, Kilindi pamoja kitwai mkoani Manyara
ambapo nyumba hizo 5000 zimejengwa kwa ajili ya wakazi hao.
“Mwamko umeongezeka kwa wananchi kujiandikisha kwa ajili ya kuhama baada ya kuelimishwa na hamasa ni kubwa sana, changamoto iliyopo ni mwananchi akijiandikisha leo anataka kuhama leo.” Amesema Bw. Nyaki
Post Comment
No comments