Breaking News

KITABU CHA KUUENZI MCHANGO WA HAYATI DKT. MAGUFULI CHAZINDULIWA JIJINI DAR

Dar es Salaam:
WATANZANIA wanapaswa kuamini kuwa, uongozi wa Dk Samia Suluhu Hassan auwezi kutenganishwa na wa hayati Dkt. John Magufuli na ndio sababu inayofanya miradi ya kimakakati kuendelea kutekelezwa kikamilifu.

Hayo yamesemwa na Mathias Kabadi wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachomzungumzia, Hayati Dkt. John Magufuli ambacho kimeandikwa na Prof Malango Chintheng kutoka Chuo Kikuu cha Hebron (UHB) nchini Malawi.

“Rais Dkt Samia, ni zao la hayati Dkt. Magufuli hivyo huwezi kuwatenganisha; ndio maana  miradi iliyoanzishwa katika uongozi wake inaendelea kutekelezwa ikiwamo ikulu ya Chamwino Dodoma, uwanja wa ndege wa Kimataifa, Msalato Dodoma, barabara za mzunguko jijini Dodoma, Bwawa la Mwalimu Nyerere, Standard Gage, Fly Overs ya Chang’ombe, daraja la Tanzanite Dar, daraja la Busisi kule Mwanza na hakuna ambao umesimama na itakamilika. 

“Mwaka 2020 niliandika kitabu kuhusu hayati Magufuli *"Mjue Dkt. John Pombe Magufuli"* kuna baadhi ya watu walihusisha suala hilo n ukabila na ukanda; kutokana na mwandishi kutoka sehemu alikotoka mhusika lakini ametokea mtu mwingine kutoka nje ya nchi ameandika kitabu kingine na leo tunakizindua,” amesema Kabadi
Amesema kuwa Dkt Magufuli ataendelea kuandikwa kutokana uongozi wake kugusa maisha ya watu hususan masikini na aliamini Afrika si masikini kutokana na rasilimali ilizonazo.

Naye mwandishi wa kitabu hicho ambacho ni cha pili kuandika kuhusu hayati Magufuli na kuzinduliwa jijini Dar es Salaam Agosti 12, 2023 Prof. Malango Chinthenga kutoka Chuo cha Hebron nchini Malawi, amesema ametumia muda wa miaka sita kukusanya taarifa mbalimbali zinazomuhusu, Dkt Magufuli, katika uongozi wake ambao umeleta chachu na mabadiliko makubwa kwa Bara la Afrika.

Kwa mara ya kwanza kitabu hico kilizinduliwa siku chache zilizopita jijini Mwanza chini ya usimamizi wa Chuo  cha St. Augustine.

Pia mgeni rasmi katika uzinduzi wa kibabu hicho, Padri Steven Musomba asema kuwa akiwamwakilisha, Askofu wa Jimbo Kuu la Dar e Salaam Grace Thaddeus, amesema kuwa elimu ambayo wamepata watanzania imeathiriwa kutokana na kutaka kufanyiwa kila kitu.

Amesema kuwa wapo wanaotaka waitwe Prof, Dkt, bila kuufanyia kazi na kusistiza kinachotakiwa kuangaliwa kwa makini ni mila, malezi kwa vijana kwa maana wengi wao wanapenda kulelewa hali inayosababisha hata ndoa nyingi kutodumu.

“Haiwezekani mtu wa nje anaamua kuandika kitabu kuhusu mtu wetu, sisi tunakwama wapi?, inawezekana ni kutokana na dharau zetu,” amesema.

Ameongeza kuwa kitabu hicho kinachoitwa ‘Africa Magufuli and Change’ ni vema kisomwe na si kuweka kabatini kwa maana kinaweza kuleta mabadiliko ya kuishi vema kwani mfumo wa maisha yetu haupo kama Ulaya, kwa watanzania ni shirikishi.

No comments