WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MGENI RASMI KONGAMANO LA VIONGOZI WA DINI JIJINI DAR
Mwenyekiti Taifa wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) Shekh Alhad Mussa Salum akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazungira (NEMC), Dkt Stanley Gwamaka akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya kongamano litakalofanyika siku ya 12 June jijini Dar es salaam.
Dar es salaam:
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano kubwa la aKitaifa la kuwajengea uelewa viongozi wa dini mbalimbali kuhusu athari zitokananzo na sauti zilizozidi Viwango katika Nyumba za ibada.
Akizungumza jijini Dar es salaam Mwenyekiti Taifa wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) Shekh Alhad Mussa Salum amesema kongamano hilo litakalofanyika Juni 12 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere( JNICC).
Amesema kupitia Kongamano hilo viogozi wa dini pamoja na viongozi wa kimila watapata elimu kutoka kwa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira NEMC juu ya kiwango gani cha sauti wanachopaswa kukitumia katika nyumba zao za ibada.
"Nitoe rai kwa Viongozi wote wa dini kujitokeza siku hiyo hili kupata elimu hiyo ambapo pia mada zipatazo tisa zitawasilishwa na kujadiliwa ikiwemo mada kuhusu Utiifu kwa Mamlaka kwa Mujibu wa Biblia pamoja na Utiifu wa Mamlaka kwa Mujibu wa Qur'an na Sunna" Alisema Shekh Mussa
Amezitaja Mada zingine kuwa ni pamoja na Uchungaji wa Haki katika Ibada na Haki za wengine Mujibu wa Qur'an (Sunna) na Biblia, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya 2004 na kanuni zake pamoja na Athari zitokanazo na Sauti zilizozidi kiwango.
Nyngine ni Usimamizi wa Mipango Miji, Uelewa kuhusu Sheria na Kanuni za Usajili wa asasi za kiraia pamoja na Majukumu na Wajibu wa RITA kwa Taasisi za Kidini.
Nae Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazungira (NEMC), Dkt Stanley Gwamaka amesema Kongamano hilo linatokana na agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye aliitaka NEMC ikutane na Viongozi wa Dini na Kimila ili kuwapa elimu kuhusu kiwango cha Sauti inayotakiwa kwenye nyumba za Ibada.
"Moja ya jukumu letu sisi NEMC ni kutoa elimu ya utunzaji wa Mazingira kwa jamii, hivyo kuna kiwango cha sauti kilichopo kisheria ambacho lazima kifuatwe ili kuweka mazingira safi na salama kwa wananchi waweze kushiriki kwenye shughuli zao za kiuchumi" Alisema Dkt. Gwamaka na kuongeza kuwa
"Hata kama una furaha au huzuni kiasi gani bado kuna kiwango cha sauti kilichopo kisheria ambacho unapaswa kutumia, hutakiwi kuweka sauti kubwa ambayo itapelekea kusababisha athari kwa wengine"
No comments