Breaking News

BRELA YAWAJENGEA UWEZO WAHARIRI JUU YA MAREKEBISHO NA MABORESHO YA SHERIA ZA KIMFUMO

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imefatoa mafunzo kwa Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari nchini kuhusu marekebisho na maboresho ya kisheria na kimfumo na utekelezaji wa kanuni za wanufaika wa mwisho kwa lengo la kuboresha huduma zinazotolewa na Wakala ili wapate urahisi wa kufanya biashara nchini

Akizungumza wakati akiwasilisha mada katika ufunguzi wa warsha hiyo ya  kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu Brela, Mkurugenzi wa Leseni, bwana Andrew Mkapa amesema wahariri ni moja ya wadau muhimu kwasababu ndiyo nyenzo muhimu inayotegemewa katika kufikisha taarifa mbalimbali kwa jamii.

“Brela inatambua umuhimu wa wahariri kuwa ni kiungo muhimu na chachu katika Nyanja ya uhamasishaji pamoja na urasimishaji biashara nchini,” Alisema Bw. Mkapa.

Alisema kwa kipindi kirefu Brela imekuwa ikishirikiana na wanahabari hususan wahariri katika mambo mbalimbali kuhusu utendaji kazi wa kila siku hususani marekebisho na maboresho mbalimbali ya kisheria na kimfumo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile ameipongeza Brela kwa kuendelea kuwashirikisha na kuwazingatia kama moja ya wadau muhimu.

Alisema Brela imekuwa ikishirikiana na wanahabari hususan wahariri kwenye shughuli zake mbalimbali zinazohusu utendaji kazi wa kila siku na pale tunapokuwa na jambo jipya na la kimkakati.

“Blera wamekuwa wakitushirikisha na kutoa taarifa kila kunapotokea marekebisho na maboresho mbalimbali yanayoendelea ya kisheria na kimfumo ili kuhakikisha kuwa tunakuwa na uelewa wa kutosha kwenye habari tunazozipeleka kwa wananchi kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara nchini,” Aliesema Bw. Balile.

Akizungumzia namna warsha hiyo itakavyowasaidia katikaa kutekeleza majukumu yao amesema maboresho yanayoendelea kwenye sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya ya huduma za usajili wa Kampuni hususan mabadiliko ya 2022 na kanuni zake.

“Niwakumbushe tu kwamba, Bunge lilipitisha marekebisho ya Sheria ya Kampuni, Sura ya 212 kwa lengo la kuwezesha upatikanaji wa taarifa za Wamiliki Manufaa katika kampuni zote ambazo zilikwisha sajiliwa na zinazoendelea kusajiliwa ili kuboresha mazingira ya uwekezaji, kuzuia ukwepaji kodi pamoja na kudhibiti utakatishaji fedha haramu na ufadhili wa vitendo vya ugaidi,” Aliongeza Bw. Balile.

Aidha, Balile amesema kuwa Brela imeshaanza utekelezaji wa ukusanyaji na utunzaji wa taarifa za Wamiliki Manufaa wa Kampuni.

“Takwimu zinaonesha kwamba, Kampuni nyingi bado hazijawasilisha taarifa hizo, hivyo basi, kwa kuzingatia umuhimu wenu kama njia muhimu ya kuwafikishia Umma taarifa, Brela wameandaa Warsha hii mahususi kwa ajili ya kupeana uzoefu na uelewa wa pamoja ili kuifikishia jamii taarifa sahihi,”amesema.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kupitia vyombo vya Habari itasaidia Watanzania kuwakumbusha juu ya muda, taratibu na umuhimu wa uwasilishaji wa taarifa za Umiliki manufaa katika kampuni mujibu wa sheria.

Mapema akiwasilisha mada katika warsha hiyo Mkuu wa Sehemu ya Usajili wa Makampuni (Brela), bwana Isdor Nkindi alieleza kuwa miongoni mwa majukumu ya Brela ni usajili wa kampuni, majina ya biashara, alama za biashara na huduma, kutoa hataza, leseni daraja la kwanza pamoja na kutoa leseni za viwanda.

Alisema warsha hiyo imekuwa ya kuhamasisha dhana ya umiliki manufaa (Beneficials owner) pamoja na kuhamasisha kuwasilisha taarifa za kila mwaka(Annual Returns) ambazo ni takwa la kisheria kwa kila kampuni au jina la biassara kuwasilsiha taarifa zake.

Bwana Nkindi aliongeza kuwa mfanyabiashara wasipo wasilisha hizo taarifa adhabu ipo kisheria ikiwemo kufutwa kwa jina la biashara hio iliyompa msajili kudhani biashara hiyo haipo tena.

“Sisi si lengo letu kufuta hizo biashara tunahamasisha kutekeleza takwa hilo la kisheria la annual returns" Aibainisha bw Nkindi.


No comments