Breaking News

TRA KILA MTANZANIA MWENYE UMRI WA MIAKA 18 LAZIMA KUWA NA TIN NAMBA KUANZIA 31 DEC

Dar es Salaam:
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesema kuwa hadi kufikia Desemba 31, mwaka huu kila Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea atatakiwa kuwa na Namba ya Mlipa Kodi(TIN) bila kujali anayo biashara au la.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na Afisa Mkuu wa Usimamizi wa Kodi nchini kutoka TRA bwana Hemed Mteri, katika semina iliyohusu masuala ya Kodi, kwa wanachama wa klabu ya waandishi wa Habari Dar es Salaam(DCPC) katika ukumbi wa Chuo cha Kodi ambapo amesema kukosa TIN namba itakuwa ni kosa la jinai.

“ifikapo Desemba 31, mwaka huu Kila Mtanzania aliyefikisha umri wa miaka 18 na kuendelea anapaswa kuwa na namba ya utambulisho wa mlipakodi(TIN) bila kujali anayo biashara ama la hadi" Alisema Bwana Mteri

Alisema kutokuwa na TIN hiyo kwa kila Mtanzania aliyefikisha umri wa miaka 18 litakuwa ni kosa la jinai. Katika kuhakikisha lengo hilo linafanikiwaTRA imeendelea kutoa elimu kwa wadau wa kada mbalimbali wakiwamo wafanyabiashara na kupitia kampeni ya ulipaji wa Kodi kwa wakati.

katika hatu nyingine bwana Mteri alibainisha kuwa TRA ina matarajio makubwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kupitia mfumo ya kidigitali ambapo imejiwekea malengo ya kukusanya Trilioni 23.1 kufikia mwishoni mwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Mapema akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA, Richard Kayombo, amesema mfumo huo wa kidijitali utasaidia kukata mizizi ya vishoka, kupunguza gharama za usafiri kwa walipa kodi.

Alisema mfumo huo pia utasaidia kuongeza mwamko mkubwa kutokana na kuwa moja ya kilio cha mda mrefu cha wananchi.

“Mfumo wa kidigitali unaonyesha kuongeza matumaini ya kufikia malengo na Kwa msaada wenu wanahabari na walipa Kodi na tunategemea ifikapo Juni 30, mwaka huu kutakuwa na habari njema,” Alisema Bwana Kayombo.

Àidha bwana Kayombo aliongeza kuwa TRA katika kuhakikisha kuwa inaboresha huduma zake hususani elimu ya ulipaji Kodi kwa makundi mbalimbali imefanikiwa kufungua ofisi katika maeneo mbalimbali nchini.

No comments