Breaking News

PROF LIPUMBA AUSHUKIA MKATABA WA KAMPUNI YA DP WORLD, ASHAURI KUFANYIKA TATHIMINI PANA KUJUA SABABU BANDARI YETU KUTOFANYA VIZURI

Chama cha wanachi CUF kimesema kuwa Mkataba kati ya Bandari Tanzania unaohusisha serikali ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai unakinzana na sheria za Tanzania hivyo Mwanasheria mkuu wa Serikali alipaswa kumshauri Rais kabla ya kuingia katika makubaliano hayo Oktoba 2022.

Akizungumza makao makuu ya chama Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Profesa Lipumba amesema mpaka hatua tuliopo ni Bunge pekee ndio linaweza kusaidia nchi kutokana na mkataba huo kukinzana na sheria za nchi pamoja na kumpa Mamlaka makubwa mwekezaji.

“Kutokana na mkataba huu Mwanasheria mkuu hakumtendea haki Rais wetu kwa sababu alipaswa kumshuri kutokanana mkataba huo unakinzana na sheria za nchi kwa kumpa mwekezaji Mamlaka zaidi kuliko Tanzania kutokana na vifungu katika mkataba huo“ Alisema Profesa Lipumba.

Ametaja moja ya vifungu ni kile kinachosema kuwa kama itatokea mgogoro wowote hautasuluhishwa hapa nchini bali utapelekwa mji wa Johannesburg Afrika Kusini na kusuluhishwa kwa kutumia sheria za kimataifa huku kikinzana na sheria yetu ambayo ilifanyiwa marekebisho kipindi Hayati Magufuli akiwa madarakani zinataka migogoro yote ya kiuwekezaji itatuliwe hapa nchini.

Profesa Lipumba amesema amepitia mkataba huo wa makibaliano kwa umakini kwa kiasi kikubwa unaelezea zaidi wajibu na majukumu ya Tanzania katika bandari baada ya uwekezaji lakini sio kwa upande wa mwekezaji.

Amesema yapo mambo mengi katika mkataba huo yanatia mashaka kutokana na upana wake na kuelezwaji wake kuwa ni bandari za Tanzania hadi kwenye maziwa hivyo hakutakuwa na mwekezaji mwingine anaeweza kuja kuwekeza katika bandari yoyote nchini hata ile ya Bagamoyo.

“Mkataba unasema ukishatoa idhini au kupitisha Mkataba huo hairuhusiwi kufanyika kwa shughuli nyingine za bandari tofauti na wao na unazuia Tanzania kujitoa, kuvunja au kufanya marekebisho kwenye Mkataba kwa aina yeyote ile hii inatia shaka sana” Alisema Profesa Lipumba

Alisema Malengo ya mkataba huu ni kuipa DP WORLD nguvu kubwa na pia utaua mradi wa Bagamoyo na eneo la kiuwekezaji la Bandari ambalo tayari limeshatengwa hii yote ni kutokana na matakwa ya mkataba huu

Aidha Profesa Lipumba aliongeza kuwa njia nzuri ya kufikia maamuzi mazuri kwa maslahi mapana ya Tanzania ni kufanyika kwa tathimini sababu za ufanisi mdogo wa bandari na kutafuta njia za kujikwamua kwa kutangaza tenda kwa sekta binafsi ili kuongeza uzalishaji wake kwa maslahi ya uchumi wa Tanzania.

“Chama cha CUF kinaamini njia nzuri ya kufikia maamuzi ni kuanza tathimini pana ya sababu kwa nini bandari yetu haifanyi vizuri baada ya kujua chanzo na hatuwezi kuiendesha kwa ufanisi ndio tuamue kuchukua kampuni za kimataifa kushindana na hatima kwa njia za kiushindani apatikane atakaye wekeza katika bandari yetu" Alisema Prof Lipumba

No comments