Breaking News

LHRC YATOA MAPENDEKEZO HAYA RASIMU YA SERA ELIMU

Dar es salaam:
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa Mapendekezo ambayo Rasimu ya Sera ya Elimu haijazingatia ikiwemo baadhi ya Taasisi kama vile Maafisa Elimu Utamaduni, Maafisa Elimu TEHAMA na Maafisa elimu wengine kutotambuliwa na rasimu ya sera licha ya nafasi hizo kuwepo katika mfumo wa elimu nchini hivyo basi wanapendekeza nafasi hizo zitambuliwe.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Wakili Anna Henga wakati akizoma mapendekezo yao kuhusu rasimi ya sera ya elimu kwa waandishi wa habari.

Wakili Henga amesema rasimu ya sera itoe ufafanuzi wa kina juu ya dhana ya elimu isiyo katika mfumo rasmi ni elimu ya namna gani ili kuondoa mchanganyiko uliopo mpaka sasa.

Alisema rasimu ya sera ielekeze ni namna gani wanafunzi waliopatia katika mkondo wa elimu isiyo rasmi watatambuliwa kwenye mfumo wa elimu rasmi.

“Rasimu ya Sera ya elimu ifungamanishwe na sera nyinginezo zinazoongelea kwa namna moja ama nyingine ujuzi na maarifa kama vile sera ya sayansi na teknolojia, sera ya viwanda vidogovidogo ili kuwa na zao la wahitimu wenye ujuzi na maarifa zaidi”. Amesema Wakili Henga.

Kadhalika, Wakili Henga amesema dhana ya elimu bila malipo iwekwe bayana kutokana na ukweli kwamba lugha iliyotumika katika rasimu inaashiria dhana ya elimu bila malipo kutokuwa bure kiuhalisia, lugha iliyotumika inaashiria dhahiri shahiri kuwa elimu haitokuwa bure bali kutakuwa na michango kadhaa.

No comments