Breaking News

BALOZI POLEPOLE AWAONYA VIONGOZI WANAOMKWAMISHA RAIS SAMIA MAPAMBANO DHIDI MALARIA.

Balozi wa Tanzania nchini Cuba Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa habari na watumishi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuulia viluilui vya mbu (TBPL) Kibaha mkoani Pwani

Pwani:
Balozi wa Tanzania nchini Cuba Humphrey Polepole kuwashitaki kwa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan wanaokwamisha mkakati wa kuhakikisha Tanzania inatokomeza Malaria ifikapo 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na watumishi mara baada ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuulia viluilui vya mbu (TBPL) kichopo Kibaha mkoani Pwani.

Balozi Polepole ambaye aliambatana na Balozi wa Cuba nchini Tanzania bwana Yordenis Despaigne amesema Tanzania kuendelea kuwa na ugonjwa wa malari huku tukiwa na kiwanda cha kutengeneza dawa ya kuua mzizi wa maambukizi ya ugonjwa huo  jambo la kujitakia.

“Melekezo ya Rais yapo bayana kupambana na malaria, Waziri Mkuu maelekezo yake yapo bayana kupambana na malaria ndiyo maana kiwanda kinaenzelea kuzalisha dawa,” amesema Balozi Polepole na kuongeza,

“Natoa rai kwa Wizara ya Afya, Tamisemi na Halmashauri zote nchini kufika hapa (kiwandani) kununua dawa kwa ajili ya kupulizwa ili tuweze kufikia malengo ya kutokomeza malaria,”.

Hivyoa Balozi Polepole ametoa wito kwa Mwaka wa Fedha ujao wa 2023/2023 kutengwa Fedha ya kutosha kwa ajali ya kununulia dawa hiyo na kuipuliza kuhakikisha viluilui vya mbu vinateketezwa na kutokomeza malaria.

Akizungumzia kiwanda hicho, amesema kinazalisha lita milioni 6 kwa Mwaka, na kusisitiza kwamba ilikuwa hadi 2025 Tanzania iwe imeshatokomeza malaria.

“Huko Cuba hakuna malaria, kwani mbu hakuna, itakuwa ni ajabu tuna kiwanda lakini bado tuna mbu, nina uhakika Rais hafurahishwi na hapendezwi na vifo vinavyotokana na malaria. Ndiyo maana masimami kiwanda kiendelee kuzalisha ila shida ni sisi wasaidizi, kuna sababu gani ya kuwa na mbu hapa Tanzania,” amesisitiza na kuhoji Balozi Polepole.

Balozi Polepole amefichua kuwa kuna mamlaka zimekuwa zikikwamisha kiwanda kwa kushindwa kusaini mkataba wa kununua dawa pamoja na kutotoa kibali kwa kiwanda kuuza dawa ya kupulizia wadudu kwenvye mimea.

Kwa upande wake Balozi wa Cuba nchini Tanzania Yordenis Despaigne amesema kwamba ushirikiano wa Tanzania na Cuba ni wa kihistoria kwa zaidi ya miaka 61 tangu kuasisiwa na waasisi wa mataifa haya.

Balozi Dispaigne amebainisha kwamba Nchi hizi zimekuwa na ushirikiano katika sekta za Afya, Elimu, Kilimo na kadhalika.

Kwamba kiwanda hicho ni alama njema ya Mashirikiano kati ya Tanzania na Cuba ambapo ameeleza kwamba kiwanda hicho kimejengwa na Cuba na mkataba wa ujenzi huo ulisainiwa Mwaka 2016 ili kuwa na kiwanda cha kutengeneza dawa ya kuua mbu barani Afrika.

Hivyo amesema hicho ni kiwanda pekee kwa bara la Afrika.

No comments