Breaking News

BENKI YA NBC YA TOA GAWIO LA BIL 6 KWA SERIKALI

Dar Es Salaam:
Benki ya kibiashara ya National Bank of Commerce (NBC) imetoa shilingi billion 6 kwa serikali ikiwa ni gawio la asilimia 30 Faida bilioni 81.9 ya taasisi hiyo .

Akizungumza katika Hafla ya ugawaji wa gawio la Serikali kutoka taasisi hiyo  Mwenyeketi wa bodi wa Benki ya NBC, Elirehema Dorie amesema kuwa benki hiyo imekuwa ikijiendesha  kutokana fedha za wanahisa ambapo benki hiyo inalenga kutoa shilingi bilioni 20 kwa wanahisa wa benki hiyo sawa na ongezeko  la asilimia 33 la faida la shilingi billion 4.5 kwa kipindi cha mwaka 2021.

"Mafanikio haya tumeyapata  mwaka jana,hii nikutokana kuwekeza katika maeneo mbalimbali yenye mchango kwa jamii ikiwemo soka ambapo tumewekeza shilingi billion1.3 tumeweza kuwekeza kwenye soka". Alisema Dorie.

Elihuruma alisema zaidi 23000 wanawake wamezeshwa kupimwa ugonjwa shingo ya kizazi ambapo shilingi milioni 500 ziweza kutumika katika utoaji wa matibabu hayo.

Alisema katika kipindi cha mwaka 2021 benki hiyo iliweza kupata faida yashilingi bilioni 81. 9 kutoka shilingi billion 60.

Kwa upande wake Msajili wa hazina Nehemia Mchechu amesema kiwango cha shilingi billion 6 cha gawio nizaidi ya Mara tatu ya mwaka jana ambapo mwakajana iliweza kupata bilioni 2 kutoka kwenye benki hiyo kama fedha itokanayo nagawio.

Alisema Gawio la bilioni 6 kwa serikali limetokana wafanyakazi wa benki hiyo kutoa huduma nzuri  kwa wateja wake.

"Ubinafsishaji una changamoto lakini pia una changamoto ambazo ni chanya  unaleta mafanikio  hadi leo hii tumeweza benki hii imeza kuchangia bilioni 6 kwa serikali".Alisema Bw. Mchechu.

No comments