Breaking News

SILENT OCEAN WAFUNGUA TAWI NCHINI INDIA

Dar es Salaam:
Kampuni ya kusafirisha mizigo ya Silent Ocean imezindua tawi jipya chini India katika jiji la Mumbai lengo likiwa ni kutatua changamoto za wafanyabiasha wanaosafirisha mizigo kutoka nchini humo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Silent Ocean, Bwana Mohammed Soloka amesema ufunguzi wa tawi hilo pamoja na kutanua huduma zake pia ni pamoja na kutokana na fursa nyingi zilizoko nchini India.

“India ni nchi ya pili duniani inayokua kwa kasi katika biashara na tuliona changamoto ya kuchelewesha kwa mizigo kufika nchini tukaamua kufungua tawi hilo na tumefanya hivyo kwa ajili ya kukuza wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa,” Alisema Bw. Soloka.

Amesema kampuni yetu siku zote ipo na wafanyabiashara nakwamba hiyo ni fursa kwa Serikali kukusanya mapato na kukuza uchumi wa nchi kupitia tawi hilo na kwasasa wafanyabishara wataweza watasafirisha mzigo yao kutoka India hadi Tanzania kwa mda mfupi wa kati ya siku 17 hadi 25.

Nae Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabishara Kariakoo, Bwana Abdalah Mwinyi amesema wanahaki ya kuwapongeza Silent Ocean kutokana na kurahisisha kufika kwa wakati mizigo ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

“Tuna kila sababu ya kuishukuru kampuni hii kwani kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita mizigo kufika nchini ilichuku muda wa miezi mitatu hadi sita" na kuongeza kuwa

“Katika siku hizi mbili tunapitia kwenye wakati mgumu tunaimani kikao cha kesho na Waziri Mkuu kitaleta matunda, tunashukuru Silent Ocean kwa kuongeza tawi lingine,” Alisema Bw. Mwinyi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wafanyabishara, Wahid Abdulghafoor amesema katika kipindi kitefu wafanyabishara wa nchi hizi mbili walikuwa na changamoto ya usafirishaji wa mizigo hivyo kwa sasa wanahitaji kufanya kazi na Silent Ocean.

No comments