UM MOTOR WAZINDUA RASMI PIKIPIKI MPYA WADAU WATOA PONGEZI KUTOKANA NA UBORA
Afisa tawala mwandamizi wa mkoa wa Dar es salaam Bibi Frola Mgonja Akizungumza leo katika uzinduzi wa pikipiki za UM motors uliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es salaam.
Mkurugenzi wa Shirika La viwango Tanzania (TBS) Dokta Athuman Ngenya akifafanua jbo katika uzinduzi pikipiki za UM motors uliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es salaam.
Dar es Salam:
Kampuni ya kimataifa ya UM motors leo tarehe 16 March 2023 imefanya uzinduzi rasmi wa pikipiki za aina ya UM uzinduzi ambao umefanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es salaam.
Akizungumza Katika hafla ya uzinduzi huo Mgeni rasmi Afisa tawala mwandamizi mkoa wa Dar es salaam, Bi. Frola Mgonja ambaye amemwakilisha mkuu mkoa Amos Makalla amesema Pikipiki za UM zimekuja kwa lengo la kuwawezesha bodaboda kujikomboa kiuchumi.
"Uzinduzi wa bodaboda hizi umekuja kusawasaidia kuwajenga kiuchumi pamoja na kutatua tatizo la usafiri Dar es salaam hii ni fursa kwa vijana wetu kutokana na kutumia mafuta kidogo kwa safari ndefu karibu km 50 kwa Lita moja" Alisema Bi.Mgonja
Awali Mkurugenzi wa Shirika La viwango Tanzania (TBS) Dokta Athuman Ngenya amesema pikipiki za UM zimethabitishwa na zinatambulikwa kwa kukidhi viwango vya ubora kwa matumizi ya usafirishaji hivyo bodaboda wachangamkie fursa kwani pikipiki za UM.
Alisema kampuni kimataifa ya UM Motor imekuwa ikisambaza na kuuza pikipiki hizo barani Amerika ambapo ina mawakala zaidi ya 1200 Ulimwenguni katika nchi zaidi ya 20.
Alisema pikipiki za UM zina ubora wa kimataifa na umezingatiwa ili kufurahishwa na kuhamasisha wanunuzi kwani umefanyika ubunifu unaopelekea Kuvuka mipaka ya uvumbuzi na pia imemuongozea hisia, starehe na furaha mwendeshaji (Bodaboda) wakati wote wa safari.
Kwa upande wake meneja masoko wa kampuni ya UM Motor bwana Elly Nyeremba Akizungumzia juu ya ubora na Muundo wa Pikipiki amesema kampuni ya UM yenye makao makuu yake nchimi Amerika ina cheti cha Shirika La kimataifa la viwango lakini imetengenezwa kukidhi na kutumika katika mazingira ya kiafrika hasa nchini Tanzania.
Alisema UM wametengeneza na kusambaza nchini pikipiki za aina tatu, mbili ni za 150 cc ambazo ni Duty max 150 cc na Max Rs 150cc na pia kuna DSRX 200cc
Pikipiki za UM ina nguvu zaidi, ina Gia tano, USB kwa kuchaji na pia ina digital dash board na zaidi mafuta yanatotumika katika safari ni mdogo mno. Pikipiki za UM zimetolewa katika matolea ya DSRX 200 cc ambayo tank linaloweza kuweka Lita 13,mafuta inatumia km 40 kwa Lita moja, sport bike nzuri kwa safari ndefu na mashambani.
Aidha bwana Nyeremba Aliongeza kuwa utengenezaji wa pikipiki ya Max Rs ambayo ina Gia tano, speed 180 km/h, tenki Lina uwezo la kuweka Lita 12,mafuta yanatumika km 50 kwa Lita, nzuri kwa matumizi binafsi, kiofisi, kusambaza vitu mbalimbali kama barua na zaidi engine oil yake bad ili baada ya km 1,000 halafu km 3,000 Kisha kila baada km 3,000.
No comments