Breaking News

MRITHI WA MREMA KUPATIKANA MARCH 6

Makao Makuu ya Tanzania Labour Party yaliyoko Magomeni usalama jijini Dar es salaam 

Dar es Salaam:
Wanachama wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wanatarajia kumchagua mwenyekiti mpya atakaye kiongoza chama hicho mpaka mwaka 2025.

Kwa mujibu wa taarifa ijiyotolewa na chama hicho Uchaguzi huo utafanyika kesho march 06, 2023 kufatia aliyekua mwenyekiti wa chama hicho Mheshimiwa Augustine Lyatonga Mrema ambaye alifariki Dunia mapema mwezi August 2022.

Taarifa hiyo imesema uchaguzi huo utarajia kutafanyika katika ukumbi wa mikutano ya Hotel ya Lego Hotel jijini Dar es Salaam kuanzia majira saa tatu Asubui.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa zaidi ya 135 wanachama kutoka Mikoa yote Tanzania bara na Visiwani wenye sifa ya kuingia katika mkutano mkuu huo watapata fursa ya kupiga kura kumchagua mwenyekiti mpya wa chama hicho .

Jumla ya wagombea saba tayali wamechukua Fomu za kugombea nafasi hiyo ambapo mpaka siku moja kabla ya kufa yika kwa uchaguzi huo (leo 5 March) jumla ya wagombea watano tayali wamerudisha fomu za kuwania kugombea nafasi hiyo.

No comments