WADAU WA SANAA WAHIMIZWA KUWASILISHA KAZI ZAO KWA AJILI YA TUZO ZA TMA 2022/23
Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) limetangaza rasmi kuwa kuanza kazi kwa mfumo wa kujiandikisha na ukusanyaji wa taarifa za nyimbo au kazi za wasanii kwa mwaka 2022 kulingana na vipengele vilivyopo tuzo za mwaka 2022/2023.
Akizungumza na jijini Dar es salaam katibu mtendaji wa baraza la sanaa nchini, Dokta Kedmon Mapana alisema mfumo huo ambao utatumika kwa uwasilishwaji taarifa za nyimbo au kazi za wasanii kwaajili ya Tuzo za musiki Tanzania ni rafiki na umezingatia kuhifadhi faragha.
"Mfumo unaotumika katika zoezi la ukusanyaji wa taarifa za kazi za wasanii ni dhabiti na umekidhi vigezo vyote hususani kuzingatia uhifadhi wa faragha (Privacy) nichukue nafasi hii kutoa wito kwa wasanii kujitokeza kwa wingi" Alisema Dkt. Mapana.
Alisema Tuzo za mwaka huu zimeboreshwa kutokana na maombi ya wadau wenyewe kwa mwaka huu kutakuwa na jumla ya vipengele 16 vyenye jumla ya Tuzo 55 ikiwa ni ongezeko la vipengele sita ambavyo ni Muziki wa Dancehall, Madj, Mtangazaji bora wa muziki katika radio.
Amevitaja vipengele vingine kuwa ni Mtangazaji bora wa muziki katika Runinga, Mtaalam bora wa Muziki na Meneja bora wa muziki.
Aidha Dkt. Mapana alingeza kuwa baraza la sanaa tanzania halina nia ya kuwashindanisha wanamuziki kwa namna yoyote bali nia yake ni kumtunza mwanamziki bora kwani tuzi hizi ni za umahili hivyo wanamziki wajitokeze kwa wingi kuwasilisha kazi zao.
Dkt. Mapana ametoa wito kwa wanamziki kiendelea kuwasilisha kazi na kujiandikisha kupitia https://tanzaniamusicawards.info pamoja na kutembelea kurasa zake za mitandao ya kijamii kupata taarifa zote kuhusu uratibu wa tuzo.
"Nitoe rai kwa wanamziki kuendelea kujiandikisha katika mfumo wa maalum na kupitia mtandao kiweza kushiriki tuzo za mwaka huu na pia nitoe rai kwa wadau kujitokeza kwa wingi kudhamini tuzo hizi" alisema Dkt. Mapana
No comments