Breaking News

MWENYEKITI WA UWT ILALA AWATAKA WANACHAMA KUJITOKEZA KATIKA KONGAMANO LA MARCH 19

Mwenyekiti wa umoja wanawake UWT WIlaya ya Ilala Neema Kiusa akiwakabidhi kadi wanachama wa UWT Kata ya Kipunguni katika ziara ya kuwashukuru wanachama
Mwenyekiti wa Umoja wanawake Uwt Wilaya ya Ilala NEEMA Kiusa akizungumza na Wanawake wa Uwt Kipunguni katika ziara ya kuwashukuru wanachama
Kaimu Katibu wa umoja Wanawake Wilaya ya Ilala Mariam Bakari akizungumza na Wanawake wa Kipunguni wakati wa ziara ya kamati ya utekekezaji Wilaya ya Ilala kuwashukuru wanachama na kuangalia uhai wa Jumuiya (aliyekaa )Mwenyekiti wa Uwt Wilaya ya Ilala Neema Kiusa.
Wanachama wapya wa umoja wanawake UWT wakila kiapo baada kuapishwa Kata ya Kipunguni wilayani Ilala katika ziara ya kamati ya utekekezaji.

Na Heri Shaaban (Ilala )
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa , amewataka Wanawake wa UWT kujitokeza kwa wingi katika kongamano la UWT Taifa viwanja vya Mnazi Mmoja Wilayani Ilala kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt,Samia Suluhu Hassan .

Mwenyekiti Neema alisema hayo katika ziara zake na Kamati ya  Utekekezaji UWT Wilaya Kata ya Kipunguni Wilayani Ilala na Kata ya Kivule  ziara ya kuwashuru Wanachama pamoja na kuangalia uhai wa Jumuiya hiyo ambapo kila Kata inajizolea Wanachama wapya .

Mwenyekiti Neema Kiusa alisema katika kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Umoja wanawake UWT  Taifa Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan .

"Nawaomba wanawake wenzangu wa Wilaya ya Ilala kujitokeza kwa wingi Katika kongamano letu siku ya Machi 19 Jumapili Viwanja vya Mnazi Mmoja tuje kuongea na Mwanamke mwezetu na kumpongeza mama jambo la mama ni letu sote "alisema Neema .

Mwenyekiti Neema aliwataka Wanawake wa UWT kupeana Taarifa  kuhusiana na kongamano hilo la UWT ambalo linafanyika Ilala .

Akizungumzia mwendelezo wa ziara ya Kamati ya utekekezaji ya Wilaya alisema dhumuni la ziara hiyo uhai wa JUMUIYA ya Umoja wanawake pamoja na kuwashukuru wanachama wao .

Mwenyekiti Neema aliwataka Wanawake kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi wa serikali za Mitaa mwaka 2024 majina yao yatapewa kipaumbele  kwa wale wanaoshiriki kazi za chama na kujitoa .

Aliwataka Wanawake wa Uwt Wilaya ya Ilala kufuata kanuni na taratibu za chama katika utekelezaji wa majukumu yao .

Wakati huo huo aliwataka Wanawake wa UWT kujitolea na kujenga   mahusiano ndani na nje ya chama hila wasifanye siasa chafu  za kupanga safu za Madiwani  na Wabunge Kwani wakati wake bado wa kupanga safu hizo kwa Sasa watumikie chama katika utekelezaji wa Ilani na kumsaidia RAIS kutangaza miradi mbalimbali ya Maendeleo

No comments