Breaking News

MSIMU WA PILI TUZO ZA TANZANIA MUZIKI AWARD WAZINDULIWA

Tamasha kubwa la utoaji wa tuzo za music nchini Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) kwa mwaka 2022/23 umezinduliwa rasmi na kushuhudiwa na wageni mbalimbali akiwemo aliyekuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam Waziri Mchengerwa ambaye amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii alisema uzinduzi huo ni faraja kwa wasanii na hata wanaoutakia mema muziki wetu.

Alisema Serikali ni itaendelea kuweka maizingira wezeshi kwa lengo la kuwasaidia wadau wa Sekta ya Sanaa, hivyo kila siku wamekuwa wakijitahidi kuwa wabunifu ndiyo maana wakaanzisha tuzo hizo ili kuwapa tahamani wasanii.

“Uzinduzi wa Tuzo za Tanzania Muziki Award utaleta faraja kwa wasanii, Sisi kama Serikali tutaendelea kuweka mazingira wezeshi ikiwemo kushirikiana na wadau wa Sekta ya Sanaa nchini, hivyo tukaona tuwe wabunifu,” Alisema Waziri Mchengerwa.

Aidha Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa viongozi watakaoendelea kuhudumu katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wafanye kazi kwa kujituma, ubunifu ili waendelee kufanya mapinduzi makubwa.

“Ni lazima tujitoe muhanga kwa kuwashika mkono vijana wenye vipaji kwa namna yoyote ile hata kama kuna changamoto za kibajeti,” Aliongeza Waziri Mchengerwa.

Kwa upande wake aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi amesema Tuzo hizo zimeletwa kwa ajili ya kubadili maisha ya wasanii nchini.

Dkt. Abbasi ameongeza kwamba Tuzo hizo zinaleta heshima ya muziki wa Kitanzania na kuongeza thamani ya wasanii wa muziki nchini.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana amesema kwa mwaka huu Tuzo hizo zitakuwa na vipengele 55 ikilinganishwa na msimu wa kwanza ambao ulikuwa na vipengele 10.

Kwamba miongoni mwa vipengele vilivyoongezeka ni pamoja na mtangazaji bora wa muziki wa Radio, mtangazaji bora wa muziki wa televisheni, Mwanataaluma bora wa muziki na Meneja bora wa muziki.

Dkt. Mapana amesema falsafa itakayotumika kupata nyimbo za kushindania tuzo hiyo ni wasanii wenyewe watatakiwa kupeleka nyimbo zao.

Picha za Matukio mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa msimu wa pili wa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) uliofanyika katika ukumbi wa ware house masaki jijini Dar es salaam.



 

No comments