Breaking News

KEMMON SPORTS AGENCY YAANDAA PAMBANO KALI KIDUNDA, TONY KUPANDA ULINGONI FEBRUARI 24

Bondia Oscar Richard na Adam mbaga wakizungumza na waandishi wa habari juu ya maadalizi yao kuelekea pambano lao la round 10 litakalofanyika siku ya 24 February katika ukumbi wa ubungo plaza jijini Dar es salaam

Bondia Halima bandola na Flora machele wakizungumza na waandishi wa habari juu ya maadalizi yao kuelekea pambano lao la round 6 litakalofanyika siku ya 24 February katika ukumbi wa ubungo plaza jijini Dar es salaam.
Dar es salaam:
Kampuni ya Kemmon Sports Agency imesema mabondia nguli wa Tanzania Seleman Kidunda atapanda ulingoni Februari 24 mwaka huu kuzichapa na Patrick Mukala raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayeishi nchini Afrika Kusini katika pambano la kimataifa litakalofanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jinini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya kuelekea pambano hilo Promota na Mkurugenzi wa Kemmon Agency Bi. Saada Kasonso amesema pambano litakuwa la ubingwa na litahusisha mikanda mitatu.

Bi. Kasonso amesema katika pambano hilo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya utangulizi ambapo hitimisho  Kidunda atazichapa na Patrick Mukala raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayeishi nchini Afrika Kusini wakiwania ubingwa wa ‘ABU’ uzito wa Super Middle.

“Wakati Tony atapambana kuutetea ubingwa wake wa ‘ABU’ uzito wa Super Bantam, dhidi ya Sabelo Ngebinyana kutoka Afrika Kusini, pia kutakuwa pia na pambano la bingwa wa TPBRC". Alisema Bi. Kasonso.

Aidha Bi. Kasonso aliongeza kuwa mbali na mapambano hayo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya utangulizi.

Amebainisha kuwa lengo la kuandaa mapambano hayo ni kuwapa hamasa vijana wanaoshiriki mchezo wa ngumi nchini.

“Kampuni ya Kemmon Sports Agency tunakuja kivingine kwa kutokufanya janja janja ambazo zimekuqa zikifanywa na kulalamikiwa na wadau wa mcgezo huu kwa kipindi kirefu kwa kutambua hilo tumejikita kukuza vipaji vya kweli Lakini vile vile tunawapa uthamani mabondia wetu,” Alisema Bi. Kasonso

Alisema mapambano hayo ya kukukata na shoka yatakutabusha mabindia wenye vipaji na sio wa mchongo.

Bi Kasonso alibainisha kuwa hadi kufikia siku ya mapambano hilo mabondia wote watakuwa wameshalipwa fedha na stahiki zao zote

Kwa upande wake bondia Tony amesema amejiandaa vizuri kwa ajili ya pambano lake na atahakikisha anashinda ili kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

No comments