Breaking News

MAADHIMISHO YA WIKI YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU KUFANYIKA MARCH 20 JIJINI DAR

Dar es Salaam:
Rais wa Chama Cha wahasibu Tanzania TAA CPA Godvictor Ibrahim Lyimo amewakaribisha wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini katika wiki ya uhasibu itakayofanyika kuanzia March  20 hadi 24 jijini Dar es salaam

CPA Lyimo amesema katika wiki hiyo ya Uhasibu kutakuwa na shughuli mbali mbali ikiwemo kutoka ushauri wa kifedha, kihasibu na jinsi ya kutunza mahesabu vizuri Kwa Wafanyabiashara na wananchi wote  Kwa jumla

Hata hivyo Chama Cha wahasibu Tanzania TAA kitatoa misaada mbali mbali Kwa makundi maalumu ya wenye uhitaji, michezo mbali mbali  Kwa ajili ya kujenga Afya pamoja na semina Kwa wahasibu na wakaguzi wa  hesabu nchini ambapo wahasibu na wakaguzi wa hesabu watapata masaa8 ya maendeleo ya kitaaluma yaani "CPd  hours" 

Wiki ya uhasibu inatarajiwa kufanyia katika maeneo ya kariakoo jijini Dar es salaam.

No comments