Breaking News

DKT. MIPAWA NA EQUICTY BANK WATANGAZA NEEMA KWA MADEREVA BODABODA

Meneja mwandamizi kutoka Equity Benki, Bwana Pascal Gallet akimkabidhi cheti cha shukrani Mkurugenzi wa Dokta Mipawa Traders Company Limited, Dkt. Salim Mipawa katika hafla iliyowakutanisha madereva wa bodaboda na wadau kwa lengo kuwaelimisha juu ya fursa zinazotolewa na EQUITY benki pomoja na kampuni ya kusambaza na kuuza bodaboda ya Hunter iliyofanyika 24 February 2023 jijini Dar es Salaam.
Meneja mwandamizi kutoka Equity Benki, Bwana Pascal Gallet akizungumza katika hafla iliyowakutanisha madereva wa bodaboda na wadau kwa lengo kuwaelimisha juu ya fursa zinazotolewa na EQUITY benki pomoja na kampuni ya kusambaza na kuuza bodaboda ya Hunter iliyofanyika 24 February 2023 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya  Dokta Mipawa Traders Company Limited, Salim Mipawa (Dokta Mipawa) akifafanua jambo katika hafla hiyo iliyowakutanisha madereva wa bodaboda na wadau kuwapatia fusra zinazotolewa na EQUITY benki na kampuni ya kusambaza na kuuza bodaboda ya Hunter iliyofanyika 24 February 2023 jijini Dar es Salaam.
Picha za matukio mbalimbali ya hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya Dokta Mipawa Traders Company Limited ilipowakutanisha bodaboda na wadau mbalimbali ikiwemo EQUITY benki na  kampuni ya kusambaza na kuuza bodaboda ya Hunter iliyofanyika 24 February 2023 jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam
Kampuni ya inayojihusisha na uuzaji na kutoa mikopo nafuu ya bodabodaa ya Dokta  Mipawa Traders  Company Limited imewakutanisha madereva bodaboda na kuwapatia mikataba ya mikopo ya gharama nafuu kuwawezesha kumiliki bodaboda zao kupitia EQUITY benki.

Akizungumza juzi Februari 24, 2023 katika mkutano huo Mkurugenzi wa Dkt. Mipawa Traders Company Limited, Dkt. Salim Mipawa amesema kampuni hiyo imejikita zaidi katika kuwasaidia vijana wa bodaboda kwa kuwapatia mikataba bora ya mikopo ya bodaboda.

“Dokta Mipawa Traders Company Limited Tumejikita zaidi katika kuhakikisha kuwa tunawatafuta wadau kwa mbalimbali wenye lengo la kutimiza ndoto za vijana wengi kuweza kumiliki bodaboda kwa kuwapatia mikataba iliyo bora, leo tumewakutanisha na Equity Benki na Hero kutimiza hilo" Alisema Dkt. Mipawa

Alisema kupitia hafla Hiyo wamiliki wa bodaboda na wote wenye lengo la kutaka kumiliki wajue namna bora ambavyo biashara inayofanywa na Equity Benki pamoja na Hero,

Dkt. Mipawa aliongeza kuwa ushirikiano huu unalenga kumfanya dereva bodaboda amiliki chombo chake hivyo kuona umuhimu wa kuwakutanisha wasambazaji wa bodaboda na watoa mikopo
 ndani ya kipindi kifupi hili kufikia lengo lao ndiyo maana .

“Lengo kuu la hafla hii ni kutaka kuwajengea uelewa madereva hawa wa bodaboda pamoja kujifunza namna ya kutunza pesa zao hususani benki ili waweze kujikwamua kiuchumi,” alisema Dkt. Mipawa.

Kwa upande wake Meneja Mahusiano wa Equity Benki, Bi Emerda Kihenga amesema benki hiyo imeamua kuja kushiriki hafla hii kutokana na kuwa imekuwa mstali wa mbele kutafuta njia rahisi ya kuwasaidia vijana kuweza kujiajili kwa kutoa mikopo nafuu hasa ya kumiliki bodaboda na bajaji.

Alisema benki hiyo imekuwa ikitoa masharti nafuu ambayi yatasaidia kila kijana kuweza kupata mkopo ya bodaboda na bajaji ni lazima awe na akaunti ya benki hiyo.

"Kijana nayetaka kumiliki bodaboda kupitia ubia huu kigezo kinachotumika ni kuwa na acount ya benki hiyo ambapo mkopaji anayehitaji bodaboda atatakiwa kuchangia sio chini ya shilingi 613,000 huku muda wa marejesho ikiwa ni miezi 12 ambapo kila mwezi ni shilingi 62,000 kwa wiki na shilingi 8,900 kwa siku.

Kwa anayehitaji mkopo wa bajaji Emerda amesema atatakiwa kuchangia sio chini ya shilingi milioni 1,780,000 kwa muda wa marejesho wa miezi 18.

“Merejesho ni shilingi 127,000 kwa wiki na shilingi 18,100 kwa siku. Muda wa marejesho wa ndani ya miezi 12, maresho kwa wiki ni shilingi 180,000 na 26,000 kwa siku,” amesema.

Kwa upande wake David Jonas ambaye ni dereva bodaboda ameshukuru mchango mkubwa wa Dkt. Mipawa katika mafanikio yake kwani hadi sasa anamiliki bodaboda tatu.

No comments