Breaking News

BRELA KUWALETA WADAU PAMOJA KUJADILIANA JUU YA SERA NA MAZINGIRA YA BIASHARA

Na Timothy Marko
Katika  Sekta ya Kibiashara Nchini wakala wa usajili wa Makapuni nchini Brela inarajia kufanya mazungumzo ya Uboreshaji wa sera za kibiashara ilkuboresha Mazingira ya ufanyaji Biashara.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar Salaam Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Ally gugu amesema kuwa Hali ya kisekta ya Biashara kati ya Tanzania na Kenya ni dola bilioni Moja Hali inayochehea Ukuwaji wa uchumi kupitia Sekta hiyo.

"Tanzania imekuwa ikiuza Bidhaa nyingi nchini Kenya Hali inayochangia nasekta ya Kibiashara kuimarika". Alisema Mhe. Gugu

Alisema siku za karibuni Hali ya Biashara kati ya Tanzania na Kenya Mipakani imezidi kuimarika.

"Mkutano wa kesho tunatarajia kujadilina juu ya fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana ili kuweza kuimarisha Sekta hii". Alisema Mhe. Gugu.

Mwenyekiti wa BARAZA la Biashara nchini Dokta Godwin Wanga amesema mkutano huo wa Tano unatarajia kuwakutanisha wa wadau wa Sekta Binafsi na Wizara ya Viwanda na Biashara.

"Baada ya Mkutano huu kutakuwa na Mikutano midogomidogo itakayohusisha Sekta Binafsi pamoja na wadau". Alisema Dk Wanga

No comments