TANESCO MKOA WA DODOMA KINARA UTEKELEZAJI MIRADI YA REA
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Dodoma Mhandisi Donasiano Shamba ameelezea mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kupitia Shirika la Umeme mkoa wa Dodoma haswa upande wa Utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza na wa pili ambapo TANESCO ndiye msimamizi wa utekelezaji wake Mkoani Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma amesema mradi wa tatu mzunguko wa kwanza umeweza kuwafikia wateja 20,319 katika vijiji 168 ambao teyari una utekelezaji wa asilimia 98.
Amesema mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili unaendelea hivi sasa kwenye vijiji 159 na unategemewa kufikia wateja 3,498 wanaotarajiwa kuunganishwa ambapo zaidi ya billioni 70.4 zitatumika kuwezesha mradi huu. Mradi umeshafikia asilimia 40 ya utekelezaji wake ambapo TANESCO Dodoma ni msimamizi wa utekelezaji huo Mkoani Dodoma.
“Mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza umeweza kuwafikia wateja 20,319 katika vijiji 168 na wigo wa mradi ni ujenzi wa njia za msongo wa kati umbali wa km 878.73, njia za msongo mdogo kilomita 1118.43 na ufungaji wa mashine 323.
Mradi una utekelezaji wa asilimia 98 na Mradi wa awamu ya tatu mzunguko wa pili una jumla ya vijiji 159 vinavyofikiwa hivi sasa unaojumuisha ujenzi wa njia za msongo wa kati wa kilometa 1617.5, njia za umeme mdogo kilometa 159 na ufungaji wa transfoma 159 na uunganishaji wa wateja 3,498 na ambapo zaidi ya billioni 70.4 zinatumika na mradi umefikia asimimia 40 ya utekelezaji wake”, amesema Meneja Shamba
No comments