NAIBU SPIKA ZUNGU AKABIDHI MSAADA WA MAJIKO YA NISHATI YA GESI KWA BABA NA MAMA LISHE WA SOKO LA KISUTU JIJINI DAR
Mbunge wa Ilala na Naibu spika wa hunge la Jamhuri ya Muungano wa tanzania mhe.Mussa Zungu amebadhi majiko ya nishati ya gesi zaidi ya 150 kwa Baba na Mama lishe wa soko la kisutu jijini Dar es salaam.
Hafla ya kukabidhi kwa mitungi hiyo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ngw’ilabuzu Ludigija ametoa pongezi kwa Mbunge wa Jimbo la Ilala ambaye pia ni Naibu Spika Mussa Zungu kwa namna ambavyo alivyo katika mstari wa mbele kutatua na kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wapiga kura wake.
“Hongera kwa kazi nzuri kwani kinachofanyika hapa leo ni kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan za kuhimiza matumizi ya nishati mbadala, hivyo mama lishe na baba lishe haya ni matunda ya maelekezo ya Rais,” Alisema DC Ludigija
Alisema nyie ndiyo wa kwanza kula matunda haya ya kuwekwa pamoja mahali rasmi pa kufanyia shughuli zenu hivyo niwatake baba na mama lishe kuwa mabalozi kwa wengine kwa kuwaeleza kuacha kufanya biashara zao barabarani kwani kufanya hivyo ni kuharibu miundombinu ya barabara.
DC Ludigija pia ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa Ilala kuhakikisha wanaitikia wito wa serikali wa wakutokufanya shughuli zao katika maeneo yaliyo rasmi.
Akizungumzia msaada huo DC Ludigija amesema matumizi ya nishati hiyo ni salama na itawasaidia itawasaidia kuongeza ufanisi katika biashara zao pamoja na kuwasaidia kuepuka matatizo mbalimbali yakiwemo ya kiafya na mazingira.
Alisema msaada huo ni rafiki na bidhaa zake zinapatikana kwa urahisi kutokana na imesambaa nchi nzima, hivyo ameipongeza kampuni hiyo kwa kuunga mkono juhudi za Rais Samia za kuhimiza matumizi ya nishati mbadala ambayo inasaidia kuepusha Taifa kuingia katika hali ya jangwa.
Kwani jambo hilo litasaidia kuokoa misitu kukatwa kwa matumizi ya kuni na mkaa.
Kwa upande wake Naibu Spika Zungu amesema kwamba wamesaidia mitungi hiyo kwa sababu baba na mama lishe wamekuwa wakihangaika na moshi kutokana na kutumia mkaa na kuni.
Aidha amesema kwamba baada ya kukaa nao hivi karibuni waliona ni bora kuwasaidia ili waweze kutumia nishati mbadala badala ya mkaa na kuni.
Naibu Spika Zungu amesema kwamba kutokana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa, takribani viwanja milioni moja vya mpira vyenye misitu vimekuwa vikiharibiwa hali inayosababisha nchi kuingia katika jangwa.
“Tumekaa na Taifa GAS kuwaomba, hivyo mitungi hii 150 inatolewa bure, lakini sharti yake gesi ikiisha utanunua kwa yule aliyekupatia, ukinunua kwingine sio uungwana,” amesema Zungu.
Zungu amewataka kutokuendelea kutumia mkaa na kuni kwani kutumia nishati hizo ni kuliumiza Taifa kwa kuliingiza kwenye ukame.
Naye Meneja wa Mahusiano Mema kutoka Taifa GAS Angel Mwita, amesema wametua msaada wa mitungi hiyo kwa kushirikiana na Mbunge wa Ilala ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia za kuhimiza matumizi ya nishati mbadala.
Amesema gesi hiyo ni salama kwa matumizi kwani inasaidia katika utunzaji wa mazingira na kwamba wana gesi ya kutosha kwa matumizi ya nchi nzima.
No comments