NEMC YAKUTANA NA WADAU KUJADILIANA CHANGAMOTO ZA TAKA NGUMU
Na. Timothy Marko
Katika kukabilianana tatizo la taka ngumu nchini baraza la Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC) kwa kushirikiana nchi washirika Zambia, Uganda na Kenya wamekutuna kujadiliana juu athari na changamoto za taka ngumu na hatua za kuchukua kuweza kukabiliana nazo.
Akizungumza na wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo Mkurugenzi wa taasisi ya Mazingira (NEMC) Dkt. Samweli Mafwenga amesema kuwa tatizo la taka ngumu limekuwa tatizo sugu Hali inayochangiwa na kuongezekakwa madampo ili kuweza kukomesha Hali hiyo taasisi hiyo inaendelea kufanya utafiti juu ya udhibiti wa taka ngumu.
"Moja ya jitihada zinazofanywa na taasi yetu ni kuhakikisha kuwa kunakuwepo na mifumo ya kisasa ya ukusanyaji wa taka ngumu kwa lengo la kuzibadili ziweze kutumika katika nyanja ya maendeleo" Alisema Dkt. Mafwenga.
Dkt. Mafwenga Alisema tayali wameshaingia makubaliano ya awali na baadhi ya majiji ya mfano ili kuweza Kufanya utafiti.
Kwa upande Wake Muwakilishi wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Bi. Hawa Mwechaga amezitaka Halmashauri zote nchini kuwa na mpango mkakati wa kutokomeza taka ngumu katika maeneo yao.
"Serikali tunapiga vita Matumizi ya mifuko ya plastic kuweza kukabilianana tatizo la uhalibifu wa mazingira pamoja na taka ngumu". Alisema Bi Mwechaga.
No comments