Breaking News

KAMPUNI YA UBER KUANZA KUTOA HUDUMA TANZANIA

Januari 18, 2023 kampuni ya UBER imetangaza rasmi kuanza kutoa huduma zake nchini Tanzania hii ni baada ya kusitisha huduma zake mapema Aprili Mwaka uliopita. 

Akizungumza katika hafla hiyo Meneja wa Uber Kanda ya Afrika Mashariki Bwana. Imran Manji amesema Tuna furaha sana  kurudi na kuendelea kutoa huduma zetu za usafiri  nchini Tanzania na tunaipongeza serikali kwa juhudi zake za kukuza huduma za usafiri wa Teksi kupitia mtandaoni.

"Tuna furaha sana  kurudi na kuendelea kutoa huduma zetu za usafiri nchini Tanzania kipaumbele chetu kwasasa ni kuwa na mfumo ambao utawasaidia madereva kutengeneza kipato cha kujikimu sambamba na kutoa usafiri wa uhakika na wa kutengemewa kwa Watanzania" Alisema Bw. Manji

Alisema kampuni ya Uber imerudisha huduma za UberX na UberXL ambazo wasafiri wanaweza kutumia katika jiji la Dar Es Salaam Uber X ni huduma ya bei nafuu ambayo inawawezesha watu wengi kufurahia huduma za usafiri wa uhakika kwenye mfumo wa UBER, Huduma za Uber XL kwa ajili ya Wasafiri sita na magari yanayotoa huduma hii yana nafasi inayotoa usafiri wa starehe na huduma hii inafaa kwa safari za familia, marafiki au msafiri anaposafiri akiwa na mizigo mingi.

Sekta ya usafiri wa teksi za mtandaoni imeleta mageuzi makubwa katika namna watu wanavyosafiri katika miji yetu na tangu mwaka 2016 UBER ilipoanza kutoa huduma zake jijini Dar Es Salaam kampuni ya uber imekua mshirika muhimu katika jiji hili kwa kutoa usafiri wa kutumia teknolojia ya kisasa kuchangia katika huduma za kiuchumi na kuwapa madereva uhuru  wa kufanya kazi kwa muda wanaoutaka sambamba na ulipaji kodi.

Aidha aliongeza kuwa kampuni ya Uber imeweka msukumo mkubwa kwenye usalama na kadri watu wanavyoendelea kutumia teksi za mtandaoni ndivyo UBER itaendelea kuwekeza kwenye usalama.

Alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa raia wengi hawana uelewa wa vipengele vya usalama ambavyo wanaweza kuvitumia wanapokua safarini Hivyo basi Uber imeanzisha kampeni inayohamasisha kuhusu usalama maarufu kama SAFETY CHECK UP.

Pia bwana Manji alisema kampeni hiyo inalenga kuimiza wasafiri kukamilisha safari zao kwa usalama, kuwasha na kutumia vipengele vya usalama vinavyopatikana kwenye mfumo wetu kama vile Uthibishaji wa PIN na kukagua taarifa za gari na dereva yaan RIDE CHECK .

"Tuna matarajio makubwa kuhusu kesho ya soko la Tanzania, Tupo tayari kushirikiana na watunga sera, kuimarisha usalama na kusaidia madereva kukuza biashara yao sambamba na kuboresha huduma kwa abiria wanaotumia mfumo wetu" Alisema Bw. Manji

No comments