CUF YAZINDUA RASMI MKUTANO YA HADHARA.. YASEMA ITATUMIA MIKUTANO HIYO KUNADI SERA, KUKOSOA NA KUSHAURI
Dar es salaam:
Chama cha wananchi (cuf) kuzindua rasmi mikutano ya hadhara leo 7 January 2023 ambapo umeudhuliwa na mwenyekiti wa chama hicho Taifa Profesa Ibrahim Lipumba Katika viwanja vya balesa Mazenze jijini Dar es salam
Mkutano huyo ulioudhuliwa na mamia ya wananchi, viongozi wa chama pamoja na wafuasi wa chama hicho kutoka maneno mbalimbali ya jiji.
Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa chama hicho Profesa Iblahim Lipumba amesema leo Tunazindua rasmi mikutano yetu ya hadhara ambayo itafanyika nchi nzima Kwa lengo la kunadi sera za chama na kuimalisha chama nchi nzima.
Mapema akizungumza wakati akimkalibisha mwenyekiti wa chama mkurugenzi wa habari (cuf) Taifa, Injinia Mohamad Ngulangwa alisema wakati huu ulikuwa ukisubiliwa kwa hamu Kufatia zuio lililowekwa kwa vyama vya siasa kutofanya mikutano ya hadhara katika kipindi cha zaidi ya miaka sita.
Alisema kipekee anapenda kutoa pongezo kwa rais Samia kutengua na kuruhusu mikutano ya hadhara kuanza tena baada ya marufuku ililokuwepo ya mtangulizi wake Rais Magufuli kwa miaka zaidi ya sita.
"Tanzania tumepitia kipindi kigumu sana hasa vyama vya upinzani ilifika wakati baadhi ya matukio na vitendo kama vile kupotea kwa watu na kuokotwa kwa maiti pembezoni mwa fukwe vilikuwa vinaongezeka lakini kufatia jitihada za mheshimiwa rais taifa imefikia mda viongozi wanakaa meza moja kuzungumzia maswala yanayohusu mustakabadhi wa taifa" Alisema Injinia Ngulangwa.
Injinia Ngulangwa aliongeza kuwa pamoja na changamoto ambazo kama taifa tulizipitia kufatia zuio hilo katika kipindi chote cha miaka sita aimaanishi kuwa tushindwe kupongeza kwa mazuri yaliyofanyika ikiwa ni pamo na kukosoa kistaarabu na kushauri inapobidi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CUF wilaya ua Ubungo bwana Bashiru Muya akizungumza katika uzinduzi huo alisema mikutano hiyo ya hadhara itasaidia kujenga vyama vya siasa sambamba na kunadi sera zao kwa wananchi.
No comments