Breaking News

TUZO ZA KUKAYE MOTO AWARDS KUFANYIKA 1 JANUARI 2023 JIJINI DAR

Mratibu wa Taasisi ya Kukaye Moto Dimateo Zion akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya maandalizi ya kufanyika kwa Tuzo hizo zitakazofanyia 1 January 2023 jijini Dar es Salaam
Mjumbe wa Kamati ya Kuratibu wa tuzo hizo  Mussa Kharid maarufu kama Mussabhai akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya tuzo hizo zitakazofanyia 1 January 2023 jijini Dar es salaam
Mjumbe wa Kamati ya Kuratibu tuzo hizo Stella Kisinga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo za KAKAYE MOTO zitakazotolewa siku ya tarehe 1 January 2023 jijini Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juu ya maandalizi kuelekea siko hiyo Mratibu wa Taasisi ya Kukaye Moto bwana Dimateo Zion alisema 
Maandalizi yote kuelekea siku ya tuzo hizo yamekamilika na kuwahakikishia washiriki kuwa zitakuwa ni tuzo bora na zenye viwango vya kimataifa.

Alisema tuzo hiyo kwa mara ya kwanza zilifanyika mwaka 2020 ambapo tuliweza kutoa Tuzo zenye muonekano wa cheti katika vipengele 15, baadhi ya vipengele hivyo ni wimbo bora wa mwaka wa Reggae, Msanii chupukizi na Mtayarishaji bora. Mwaka 2021 Tuzo hazikufanyika kwasababu za Taasisi kuendelea kufanya maboresho.

“Mwaka 2022 Tuzo hizi zimerejea tena kwa awamu ya pili ambapo tumejitahidi kuweka maboresho ya kuongeza vipengele pamoka na vigezo vitakavyomuwezesha mshiriki kuweza kishindana,” Alisema bw Zion

Alisema tuzo za mwaka zimeboeshwa zaidi na zitakuwa katika muonekano wa kipekee kwani kutakuwa na Tuzo za trophy katiKa muonekano wa aina mbili tofauti pamoja na cheti.

"Awamu hii kutakuwa na vipengele zaidi ishirini na utoaji tuzo utakuwa katika hadhi tatu yaani daraja la kawaida, daraja la kati na daraja la juu" Alisema Bw. Zion

Alisema lengo kubwa la utoaji wa tuzo hizo ni kuendelea kutoa motisha kwa wafanyaji wa muziki huu, kuupa thamani pamoja na kufungua fursa kwa wadhamini pamoja na wasanii kuweza kufanya kazi kwa pamoja

Aidha amevutaja baadhi ya vipengele ambavyo vitashindanishwa katika tuzo hiyo kuwa ni mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka za Reggae na Dancehall, Video bora ya mwaka, muongozaji bora wa vido wa mwaka na msanii wa kike na kiume chipukizi.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Uratibu wa tuzo hizo bwana Mussa Kharid maarufu kama Mussabhai ameomba wadau wakiwemo vyombo vya habari kuendelea kuunga mkono muziki huo nchini.

Mapema mmoja ya mjumbe wa maandalizi ya Tuzo hizo Bi. Stella Kisinga amesema Muziki wa Reggae umeanza miaka mingi sana, na wasanii wa muziki huu nchini wamekuwa wakifanya makubwa lakini hawatambuliki.

Alisema katika kuhakikisha wasanii wa mziko huo wanatambulika na kupata heshima wanayostahili tayali wameanzisha chama ambacho kitakachowatambua na kuufanya muziki huu kupiga hatua zaidi.

No comments