Breaking News

WAZIRI MAJALIWA KUFUNGUA KONGAMANO LA 15 WADAU WA SETELAITI ZA HALI YA HEWA BARANI AFRIKA

Waziri mkuu kasimu majaliwa anategemewa kufungua kongamano la 15 la wadau wa setelaiti za hali ya hewa za shirika la  EUMETSAT barani afrika "15 EUMETSAT USSER FORUM IN AFRIKA" utakaofanyika siku ya tarehe 13 hadi 16 jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) imesema kuwa katika kongamano hilo  wadau wa hali ya hewa wanaotumia teknolojia ya  setelaiti za hali ya hewa kwa nchi wanachama wa WMO ikiwepo tanzania watajadiliana juu ya kuboresha na kuzipatia ufumbuzi changamoto wanazokutana nazo.

"Kupitia kongamano hilo nchi wanachama zitanufaika na uboreshaji wa utabiri wa hali ya hewa utakaosaidia kupanga mipango ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii"

Taarifa hiyo imeongeza kuwa mkutano huo wa siku mbili wenye kauli mbiu ya " Kuelekea kizazi kipya cha setelaiti za hali ya hewa afrika" umeratibiwa na taasisi ya kimataifa ya  EUMETSAT inayoshirikiana na shirika la hali ya hewa dunia (WMO) katika shughuli za ungazi wa hali ya hewa kwa kutumia setilite.

No comments