Breaking News

TUJITOKEZE KWA WINGI KUPIGA KURA

Albert Chalamila ametoa wito kwa wakazi wa Jijini la Dar es Salaam kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27/2024 kufika kwa wakati katika vituo vya kupiga kura kwani baada ya saa 10 jioni hatoruhusiwa mtu mwingine kupiga kura isipokuwa waliopo kituoni.

Hayo amesema leo Novemba 25, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali ambapo amewasisitiza wananchi kuzingatia miongozo ya Uchaguzi.

“Niwaombe wakazi wa Dar es Salaam kuzingatia taratibu na miongozo ya uchaguzi Ili watimize haki yao ya Msingi ya kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka, mtu yeyote akifika Saa kumi hata ruhusiwa kupiga kura bali tu wale ambao wapo kwenye mstari kituoni” Amesema RC Chalamila

Amesema tarehe 27 Novemba 2024 Kila aliye Mtanzania anashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji na vitongoji kwa kuchagua wenyeviti na wajumbe wake ambapo mkoa wa Dar es Salaam una jumla ya mitaa 564,

Aidha amesema kuwa kwa mujibu wa Sensa iliyopita mkoa wa Dar es Salaam una jumla ya watu zaidi ya Milioni 5 na laki tatu kwa mantiki hiyo watu waliofika miaka18 ni mil 3 kwa hiyo kwa mitaa yote inatarajiwa kuwa na wenyeviti na wajumbe.

Rc Chalamila ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha watu kujitokeza kwenda kupiga Kura ambapo amewasisitiza wakazi wa Dar es Salaam  kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga Kura na kuchagua viongozi wanaowafaa.

Hata hivyo Rc Chalamila amesema kuwa mara nyingi kumekuwa na malalamiko machache kwamba mchakato wa Uchaguzi imekua na taarifa zilizofichama na kusababisha baadhi ya wenzetu kushindwa kupata na kujiandaa na Uchaguzi.

“Naamini wale wapenzi wa vyama vingi watajitokeza kupiga kura na kudumisha demokrasia iliyopo na kuchagua viongozi bora ili kujiletea maendeleo”.Alisema Rc Chalamila.

Ameongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anahimiza matumizi ya 4R lazima tujenge siasa njema,siasa ambazo tunakaa pamoja na kuziepuka zile siasa za chuki,

Rc Chalamila ametoa rai kwa wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kwenye Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa ambapo itakuwa ni salamu kwa mataifa mengine Duniani kwamba Tanzania imeshavuka kihunzi cha demokrasia kwamba kila aliejiandikisha anapiga kura.

Rc Chalamila alisema inajulikana kuwa na Uchaguzi sio kigezo cha kuwa na demokrasia bali Uchaguzi unatakiwa kuwa wa wazi na kwa mantiki mhe Rais Samia Suluhu Hassan anataka Uchaguzi uwe huru na haki na ambao unaoakisi zile 4R alizoziasisi.

Sanjari na hayo Rc Chalamila alisema siku za kujiandikisha zilikuwa nyingi ila siku ya kupiga kura ni moja,hapa unaweza ukajiuliza kama una vituo vya kujiandikisha 1800 na wananchi wakatumia siku 5,6 mpaka 7 ila itumike siku 1 kupiga kwa idadi hiyohiyo Waliojiandikisha,

Vituo Vya kupiga kura hiyo siku ya tarehe 27 ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa vimeongezwa ili kuhakikisha kila mmoja anapata nafasi ya kupiga kura na hali ya usalama katika Jiji la Dare es salaam ipo vizur na vyombo vya ulinzi na usalama vimejiandaa vizur.

No comments