Breaking News

TIGO SASA YAITWA YAS

Honora Tanzania public limited (Tigo) na Honora Tanzania mobile solution Limited (Tigo pesa) ambazo ni sehemu ya kampuni ya AXIAN Telecom Group zimetangaza mabadiliko makubwa ya chapa ambapo tigo itajulikana rasmi kama Yas , huku huduma zake za kifedha ,tigo pesa zikibadilishwa kuwa MIXX by YAS.

Mabadiliko haya ya chapa ni sehemu ya mpango mkakati wa AXIAN Telecom wa kuunganisha makampuni yake yote ya mawasiliano barani Afrika kuwa chini ya chapa moja ya YAS na MIXX by YAS kama alama ya nguvu ya pamoja na mafanikio.
YAS na MIXX by YAS zinalenga kuakisi maono ya kampuni ya kuwa kiini Cha mapinduzi kidijitali na fedha barani Afrika kupitia suluhisho za kisasa za kidijitali na fedha chapa hii mpya zinalenga kuboresha mawasiliano ya mamilioni ya watanzania kutoa fursa mpya zisizo na kikomo.

Akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini dar es salaam Leo mchana waziri wa habari mawasiliano na Technolojia ya habari mheshiwa Jerry Silaa amesema uzinduzi wa brand hiyo itaunganisha nchi za kiafrika na kuendelea kuweka msingi wa utekelezaji wa uchumi wa kijiditali katika taifa letu.
Nchi hizo ni Madagascar, commoro , Senegal ,Togo na Tanzania.

Aidha amesema matumizi ya tehama, internet yameongezeka hivyo brand mpya ya YAS  itashirikiana na brand zingine zilizopo kwenye soko ili kuweza kumsaidia  mtanzania kuongeza mawasiliano.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya YAS Tanzania Rostam Aziz amesema mabadiliko hayo yanaonesha dhamira ya kuendelea kuwekeza na kuleta mageuzi kijiditali nchini Tanzania bara na visiwani.

Naye mwenyekiti wa bodi ya AXIAN Telecom Group Hassanein Hiridjee amesema kampuni hiyo imekuwa katika safari ya kipekee ya kuunganisha watu barani Afrika na kupanua wigo wa huduma zake.




No comments