Breaking News

TMA: MSIMU WA VULI UTAKUWA NA MVUA ZA CHINI YA WASTANI HADI WASTANI KATIKA MAENEO MENGI YA NCHI

Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari kuanza kwa rasmi utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2022

Dar es Salaam;
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2022 kwa maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka.

Akizungumza wakati wa mkutano na vyombo vya habari katika Makao Makuu ya TMA, Ubungo Plaza, Tarehe 2/9/2022, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi alisema maeneo ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua yanatarajiwa kupata mvua za chini ya wastani hadi wastani.

“Kutokana na mifumo ya hali ya hewa ilivyo kwa sasa na inavyotarajiwa katika kipindi chote cha msimu, kwa ujumla kutakuwa mvua za chini ya wastani hadi wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka"Alisema Dkt. Kijazi.

Alisemu Msimu unatarajiwa kuanza kwa kuchelewa na kuambatana na mtawanyiko wa mvua usioridhisha, Ambapo Vipindi virefu zaidi vya ukavu vinatarajiwa katika miezi ya Oktoba na Novemba 2022.

Dkt. Kijazi aliongeza kuwa kutakuwa na vipindi vya ongezeko kidogo la mvua vinatarajiwa kujitokeza katika maeneo machache hususan wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Disemba 2022. 

"Kwa kawaida msimu wa mvua za Vuli huisha mwezi Disemba. Hata hivyo, kunatarajiwa kuwepo na muendelezo wa mvua kwa mwezi Januari, 2023”. Alieleza Dkt Kijazi


 

No comments