Breaking News

ACT-WAZALENDO YATANGAZA MAAZIMIO YA KIKAO CHA HALMSHAURI KUU

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimetangaza maadhimio makuu yaliyoazimiwa katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho uliofanyika Septemba 4 jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo Janeth Joel Rithe, amesema kikao hicho kwa kayulu moja kipendekeza azimio la kwanza ni kuhusu Ofisi za Makao Makuu ya Chama.

Alisema halmashauri Kuu ilipokea Taarifa ya Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Chama kwa upande wa Bara na Zanzibar.

"Katika kikao cha Halmashauri Kuu kimepongeza hatua iliyofikiwa sasa ya kupatikana kwa Ofisi ya Wasemaji wa Kisekta (iliyopo Oysterbay, Dar es salaam) pamoja na Ofisi ya Makao Makuu (iliyopo Magomeni, Dar es salaam) iliyopewa jina la Jengo la Maalim Seif kumuenzi Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama chetu,” alisema Rithe.

Alisema Halmashauri Kuu imetoa mapendekezo kwa Sekretarieti kuwa uzinduzi wa Ofisi Mpya ya Makao Makuu uandaliwe na kufanyika mapema iwezekanavyo.

Ametaja azimie la pili ni Uchaguzi wa Ndani ya Chama ambapo kikao Halmashauri Kuu imepitisha ratiba ya Uchaguzi huo kwa ngazi za Matawi, Kata, Majimbo, mikoa na Taifa ambao utafanyika kuanzia Machi 2023 hadi Machi 2024.

Alizungumzia azimio la tatu kuhusu Taarifa ya Wasemaji wa Kisekta ambapo amesema Halmashauri Kuu imepokea Taarifa ya Miezi Sita ya Utendaji wa Kamati ya Wasemaji hao iliyowasilishwa na Waziri Mkuu Kivuli Dorothy Semu.

Alisema Halmashauri Kuu pia imeipongeza Kamati ya Wasemaji wa Kisekta kwa kazi kubwa inayoifanya ya kuwasemea Watanzania.

"Halmashauri Kuu imeagiza Kamati ya Wasemaji wa Kisekta kupaza sauti juu ya maeneo mahsusi ya kukithiri kwa tozo za Serikali, uvunjifu wa haki za binadamu magerezani, changamoto za bima ya afya na umuhimu wa hifadhi ya jamii na mageuzi katika Jeshi la Polisi" Alisema bi Rithe.

Aidha bi rithe aliongeza kuwa   kuhusu Usimamizi wa Uwajibikaji wa Serikali ya Zanzibar, amesema Halmashauri Kuu imepitisha Azimio la kuundwa kwa Kitengo cha Chama cha Kusimamia Uwajibikaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (Government Oversight Unit).

Kitengo hicho kitakuwa na majukumu ya kufuatilia kwa karibu uwajibikaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kutoa sera mbadala,

Akizungumzia azimio la tano la ambalo ni kuhusu Sera ya Wamachinga (Madhila ya Wamachinga), alisema Halmashauri Kuu ya Chama Taifa imepitisha Sera ya Chama ya Wamachinga inayoangazia kutatua madhila na changamoto zinazowakabili wamachinga na hatua za kisera zinazopaswa kuchukuliwa kukabiliana na changamoto hizo.

Bi rite alibainisha kuwa kikao cha Halmashauri Kuu tayali imeielekeza Sekretarieti kupanga uzinduzi wa sera hiyo.

Azimio la sita kuhusu Ujenzi wa Chama ni kuwa Halmashauri Kuu ya Chama imepokea Taarifa ya Ujenzi wa Chama kwa kipindi cha miezi sita iliyopita na kupitisha Program ya Ujenzi wa Chama ya Mwezi Septemba-Novemba 2022.

“kikao icho kimepokea Taarifa ya Ujenzi wa Chama kwa kina (intensive party building) kwenye Mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Ruvuma, na Tanga uliofanyika katika miezi sita iliyopita, Halmashauri Kuu imeelekeza ujenzi wa Chama kwa kina kwenye mikoa ya Magharibi (Tabora, Katavi, Kigoma na Shinyanga) na Pwani/Kusini (Pwani, Lindi, Mtwara na Mkoa wa Kichama wa Selous) na Mikoa yote ya Kichama ya Zanzibar,” alifafanua bi rithe.

Aidha kikao hicho pia kilipokea taarifa za mageuzi ya Uendeshaji wa Chama Kisasa (Modernisation of the Party) ni kwamba Halmashauri Kuu ya Chama imepokea Taarifa ya Mageuzi ya Uendeshaji wa Chama Kisasa kupitia mfumo wa ACT Kiganjani na kutoa maelekezo mahsusi ya kuendelea kujiimarisha katika utumiaji wa njia za kidijitali katika uendeshaji wa Chama.

Alisema halmashauri Kuu ya Chama imepitisha Ahadi ya Chama kwa Watanzania (Brand Promise) na kuelekeza Sekretarieti ya Chama kuandaa uzinduzi wake utakaofanyika Bara na Zanzibar mapema iwekeanavyo.

Aidha bi rithe aliongeza kuwa  Halmashauri Kuu ya Chama, kufuatia mapendekezo yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa Juma Duni Haji, imeidhinisha uteuzi wa Wajumbe wa Halmashauri Kuu mbapo ni Ally Abdullah Saleh (Alberto), Mkunga Hamad Sadalla, Suleiman Said Bungara (Bwege), Nyangaki Shilungushela, Rehema Khamis Haji na Pendo Dominick Manyanya.

Huku Wajumbe wa Kamati ya Maadili Taifa wakiwa ni Ussi Khamis Haji (Mwenyekiti), Juma Khamis Juma (Mjumbe), Naibu Katibu Ngome ya Vijana Zanzibar na Mohamed Khamis Bussara.

No comments