Breaking News

WAZAIRI UMMY: JUMLA YA WATOTO 1,363,834 KUANZA DARASA LA AWALI 2022

Takwimu za maoteo ya uandikishaji wa wanafunzi wa Darasa la Awali zinaonesha kuwa jumla ya wanafunzi 1,363, 834 (wavulana 676,028 na wasichana 687,806) wanatarajiwa kuandikishwa ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi 1,198,564 (wavulana 604,995 na wasichana 593, 569) walioandikishwa 2021  Idadi hii inajumuisha Wanafunzi wenye mahitaji maalum 6,376 wakiwemo Wavulana 3,277 na Wasichana 3,099.
 
Uandikishaji wa wanafunzi wa Darasa la Awali ulianza Novemba, 2021 na unaendelea. Hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2021 jumla ya wanafunzi 488,780 wa Darasa la Awali wakiwemo wasichana 247,003 na wavulana 241,777 sawa na asilimia 35.93 ya wanafunzi wote wanaotarajiwa kuandikishwa darasa la Awali, waliandikishwa katika shule za serikali . Idadi hii, inajumuisha wanafunzi wenye mahitaji maalum 1,232 ambapo wasichana ni 642 na wavulana 590.
Uchambuzi wa takwimu hizo unaonesha kuwa, Mikoa 5 ambayo inaongoza kwa uandikishaji ni Manyara (57.99%), Mara (49.37%), Njombe (49.00%), Tanga (47.85%) na Mbeya (46.99%). Aidha, mikoa 05 ambayo takwimu za uandikishaji zipo chini ni Mwanza (21.17%), Dar es Salaam (20.44%), Mtwara (19.52%), Rukwa (17.33%) na Katavi (8.39%). Takwimu hizo, zinaonesha kuwa, Mkoa wa Manyara pekee ndio una uandikishaji wa wanafunzi wa Darasa la Awali zaidi ya asilimia 50

No comments