Breaking News

CHALINZE WAKAMILISHA UJENZI WA MADARASA, WAMPONGEZA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KWA FEDHA ZA MAENDELEO

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Zainab Abdallah akionesha  taarifa ya Halmashauri ya Chalinze ya ukamilishaji wa vyumba 80 vya madara kwa fedha za maendeleo zilizotolewa na Rais. Kulia kwake Mbunge wa Chalinze, Mh. Ridhiwan Kikwete na Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Chalinze, Ramadhan Possi
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Zainab Abdallah akipokea taarifa ya Halmashauri ya Chalinze ya ukamilishaji wa vyumba 80 vya madara kwa fedha za maendeleo zilizotolewa na Rais. Kulia kwake Mbunge wa Chalinze, Mh. Ridhiwan Kikwete na wajumbe wa CCM. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Chalinze, Ramadhan Possi pamoja ba Diwani wa Kiwangwa

Mbunge wa Chalinze, Mh. Ridhiwan Kikwete akitoa shukrani kwa niaba ya Wananchi wa  Chalinze kwa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan kwa fedha za maendeleo ndani ya Halmashauri hiyo ya Chalinze.

NA MWANDISHI WETU, CHALINZE.

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwan Kikwete amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha fedha za maendeleo kwa Wana Chalinze kiasi cha Bilioni 1.7.

Mh. Ridhiwan Kikwete amesema, kazi inaendelea ya kujenga maendeleo ya Watu huku akitoa shukrani za Wana Chalinze kwa Mh. Rais Samiah Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali maisha ya Watanzania anaowaongoza.

"Kazi yetu ni kuhakikisha Ndoto na Maono yake yanatimia

Chalinze Tumekamilisha Tarehe 4 January 2022, ilikuwa siku nzuri sana kwa wananchi wa Chalinze baada ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kupokea vyumba vya madarasa 80 yakiwemo Madarasa ya sekondari 66 na Shule ya Msingi Shikizi 14 kwa upande wa Elimu.

Na kuongeza kuwa; 

"Milioni 80 kwa ajili ya Bweni la wanafunzi wenye uhitaji maalum shule ya msingi Chalinze huku Milioni 90 Nyumba ya Mganga Tatu kwa Moja Hospitali ya Wilaya Chalinze inayojengwa Msoga kutoka kwenye Fedha za Uviko." Alisema Mh. Ridhiwan Kikwete

Alisema kuwa, miradi mbali inaendelea kujengwa na mingine imekamilika kupitia fedha hizo za Maendeleo Bilioni 1.7 zilizotolewa na Mh. Rais Samia


No comments