Breaking News

WAITARA ATOA MAAGIZO MATANO LATRA

NAIBU wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara ametoa maagizo matano kwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ikiwamo kuwatoza faini ya sh. 500,000 watoa huduma wa usafiri wanaokiuka sheria ya mamlaka hiyo.

Pia aliitaka LATRA kuhakikisha  watoa huduma wanaopigwa faini na kurudia makosa yaleyale wanawapeleka mahakamani  pamoja na kuwanyima leseni ya kuendelea kutoa huduma hiyo.

Waitara aliyabainisha hayo Jijini Dar es Salaam katika kikao maalumu na watendaji wa LATRA akitaka kufahamu namna mamlaka hiyo ilivyojipanga kutatua changamoto sekta ya usafiri ardhini.

Alisema wapo watoa huduma  usafiri ardhini ambao wamekuwa na utaratibu wa kupandisha nauli kinyume na utaratibu,mabasi kukatisha tiketi huku yakiwa yamejaza na abiria kukatiwa tiketi ya basi  ambalo halipo kituoni.

“Ni lazima LATRA  wahikikishe wanajipanga kuwasaidia abiria ili wasiongezewe nauli lakini pia mtu anapokata tiketi basi wakala au kampuni husika wahikikishe gari linakuwepo.

 "Tiketi zimekuwa zinauzwa hadi mtaani, mawakala wamekuwa wakijipangia bei hadi mara mbili ya bei iliyoainishwa kwa kipindi hiki ambacho shule zinafunguliwa Latra jipangeni kudhibiti vitendo hivi mikoa yote,"

“Hizi faini za sh.250,000  zimekuwa chache, naelekeza  faini iwe sh 500,000 na wale ambao watatozwa fedha hizo na kurudia makosa yale yale wapelekwe mahakamani,’’alisema

Agizo la pili ambalo Waitara alilitoa kwa mamlaka hiyo, ni kuwataka kuunda kikosi kazi maalumu itakayofatilia upandishaji holela  wa nauli ili kudhibiti utaratibu huo na  kuwaondolea kero abiria.

Pia Waitara alieleza changamoto  wanayopitia abiria wanaotumia usafiri wa treni ikiwamo kupandishiwa  nauli za tiketi kiholela.

‘’Watu wanawahi kukata tiketi wanakaa nazo baadae wanauza kwa feha nyingi, au abiria anaambiwa mfumo unasumbua baadae anauzia kwa gharama ya juu nina ushahidi wa kutosha, sektaya usafirishaji in changamoto nyingi,’’alisema.

Waitara alihitimisha kwa kuitaka LATRA kuhakikisha wasafirishaji wakati wote wanafuata utaratibu  bilakujali ni wakati wa sikukukuu  akiewaelekeza kuwa na  madaraja  ya kuwatenganisha wasafirishaji wanaowasumbua  na wale wanaozingatia sheria.

Akieleza namna LATRA ilivyojipanga kutatua kero za usafiri hasa za upandishaji holela wa nauli Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara wa Mamlaka hiyo  Johansen Kahatano, alisema  punde mfumo wa tiketi mtandao utakapoanza kutumika utaondoa adha hiyo kwani abiria atakuwa akikata tiketi kwa njia ya mtandao bila kulanguliwa.

Akizungumzia uundaji wa kikosi kazi kwa ajili ya kuboresha utendaji wa mamlaka Kahatano alisema tayari wamepata muundano wa utendaji wa mamlaka hiyo hivyo wamekusudia kuajiri watumishi wengi zaidi.

Alisema LATRA wamejipanga kuhakisha wanafunzi wanaorudi mashuleni Januari 12-15 hawapitii changamoto za usafiri

No comments