WAKILI ANDREW KEVELA AJITOSA KUWANIA USPIKA WA BUNGE
Mkurugenzi wa sheria wa kampuni ya Yono Auction Mart wakili Andrew Stanley Kevela leo january 14, 2022 amechukua fomu kuomba kuteuliwa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu siku moja kabla ya kufungwa kwa zoezi la kuchukua fomu na kurudisha zoezi ambalo litamalizika kesho January 15, 2022.
Alisema anatambua kuwa nafasi hiyo nyeti ya uspika wa bunge ameamua kuchukua fomu akiwa kama mwanachama wa CCM na kutokana na kuona mwenendo wa serikali chini ya Rais Samia Suluhu kuwapa kipaumbele vijana na kuwataka kuwania nafasi mbalimbali za uongozi pindi zinapotokea.
"Rejea kauli ya mhe rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kuonyesha katika kipindi kifupi tangu kuingia madarakani amekuwa akitoa kipaumbele kwa vijana kwa kuwateua katika nafasi mbali hivyo kunipa hamasa kama kijana kugombea nafasi hii" Alisema Wakili Kevela.
Wakili Kevela aliongeza kuwa kama kijana ana matumaini makubwa kushinda hivyo kumsaidia mheshimiwa rais kutatua kero mbalimbali za wananchi na kuliletea taifa maendeleo.
"Nina uzoefu mkubwa katika maswala ya sheria hiyo ntatumia uwezo nilionao kuliendesha bunge kuisaidia serikali kutatua kero na kuishauri serikali kuweza kuwaletea maendeleo wananchi na Taifa kwa ujumla" Aliongeza Wakili Kevela.
Katika hatua nyingine wakili Kevela amezishauri taasisi mbalimbali nchini kutoa nafasi kwa vijana katika nafasi mbalimbali hususani uongozi kwa lengo la kuwawezesha vijana kutoa mchango wao katika kukuza uchumi wa taifa.
No comments