Breaking News

MBUNGE WA MWANGA JOSEPH TADAYO AJITOSA MBIO ZA KUWANIA USPIKA

Mbunge wa Jimbo la Mwanga, mhe. Joseph Tadayo Akipokea fomu ya kugombea kiti cha Uspika kutoka kwa Katibu Mkuu Msaidizi idara ya Oganaizesheni, Bw. Solomon Itunda.
Mbunge wa Jimbo la Mwanga, mhe. Joseph Tadayo akisaini kitabu cha kumbukumbu akishuhudiwa na Katibu Mkuu Msaidizi idara ya Oganaizesheni, Bw. Solomon Itunda ofisi ndogo CCM lumumba jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
Mbunge wa Jimbo la Mwanga, mkoani Kilimanjaro Joseph Tadayo leo January 13, 2022 amechukua fomu kuomba kuteuliwa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu amesema amechukua fomu kugombea nafasi hiyo kutokana kuwa na sifa zinazotakiwa zinazokidhi pamoja na kutimisha takwa la katiba.

"Leo nimefika kuchukua fomu kuomba ridhaa ya kuteuliwa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge  la jamhuri ya muungano wa Tanzania" Alisema mhe Tadeyo. 

Alisema nimeamua kuchukua fomu ya kugombea nafasi hii ya uspika wa wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kufatia kuona ninavyo vigezo pamoja na kutumia nafasi yangu kikatiba.

No comments