Breaking News

UJENZI WA RELI YA SGR DAR - MOROGORO WAFIKIA ASILIMIA 95

Timothy Marko.
Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini Masanja Kadogosa amesema kuwa ujenzi wa Reli ya kisasa ya standard Gauge kutoka Dar es Salaam Hadi Morogoro  umefikia Asilimia 95.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wahabari jijini Dar es Salaam Masanja Kadogosa amesema kuwa ujenzi wa kipande cha Morogoro Hadi Makutupora umefikia Asilimia 77wakati kipande cha Mwanza isaka ni Asilimia nne.

"Kipande cha Makutupora Hadi Tabora mkataba wake tayari umeshasainiwa mwezi Desemba na ujenzi unaendelea". Alisema Kadogosa.

Kadogosa Aliongeza kuwa wananchi wanaweza kupata taarifa za Mradi huo kupitia tovuti ya shirika Hilo www.trc.co.tz
 

No comments