Breaking News

MWANDISI HHAYUMA ACHUKUA FOMU KUUTAKA USPIKA, WATIA NIA WAFIKIA 49

Ikiwa zimebaki siku mbili kufungwa mchakato Mbunge wa Jimbo la Hanang, mkoani Manyara Mhandisi Samwel Hhayuma leo January 13, 2022 amechukua fomu kuomba kuteuliwa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu amesema aamechukua fomu kugombea nafasi hiyo kutokana kuwa na sifa zinazotakiwa.

"Leo nimefika kuchukua fomu kuomba kuteuliwa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge  la jamhuri ya muungano wa Tanzania"

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu
msaidizi idara ya Oganaizesheni, Bw. Solomon Itunda amesema jumla ya wanachama 49 wamejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo mpaka leo Alhamisi Januari 13, 2022.

Aidha bw. Itunda amewataka wanachama wote ambao wamechukua fomu kutumia siku mbili hizi kati ya kesho na kesho kutwa kukamilisha mchakato huo na kuwatoa wasiwasi kuwa kiwa na imani kwani haki itatendeka na anayestahiki atapewa
Mbunge wa Jimbo la Hanang, mkoani Manyara Mhandisi Samwel Hhayuma mara baada ya kuchukua fomu kuomba kuteuliwa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ofisi ndogo Lumumba Jijini Dar es salaam.
 

No comments