Breaking News

MKEMIA MKUU BADO KUNA CHANGAMOTO USAFIRISHAJI WA KEMIKALI HATARISHI NCHINI

MKEMIA Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko amesema kuwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imebaini kuwepo kwa changamoto katika usafirishaji wa kemikali hatarishi nchini.

Dkt. Mafumiko alibainisha hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua kikao cha wadau wanaosafirisha kemikali hatarishi.

Alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni madereva kusafirisha kemikali bila kuwa na mafunzo ya usafirishaji salama wa kemikali, upakiaji na upakuaji wa mizigo ya kemikali hatarishina ambazo zilishatolewa maelekezo ya usimamizi wake kufanyikapasipo kuwepo na wakaguzi.

Changamoto nyingine alisema ni wasafirishaji kutokuwa na vibali vyausafirishaji, mizigo ya kemikali kuchanganywa na vitu vingine kama vile chakula na mkaa, ukosefu wa sehemu maalum zakuegesha magari yaliyobeba kemikali na ubovu wa baadhi yamagari yanayotumika kusafirisha kemikali kama Sheria inavyoelekeza.

“Mamlaka imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kutatua changamoto hizo wakati wa usafirishaji wa kemikali hatarishi,”.

“Jitihada hizo ni pamoja na kutoa mafunzo kwa madereva juu ya usafirishaji salama wa kemikali; kuandaa miongozo ya usafirishaji wa kemikali hatarishi na kushirikiana na wadua mbalimbali katika kutatua changamoto ambazo ziko nje ya majukumu ya Mamlaka,” alisema.
Akizungumzia kuhusu kikao hicho Dkt. Mafumiko alieleza kuwa ni sehemu ya jitihada za Mamlaka kuendelea kuboresha utekelezaji wa Sheria ya kemikali hasa katika eneo la usafirishaji salama wa kemikali hatarishi.

“Tutajadili na kubadilishana uzoefu wa namna ya kutatua changamoto husika kwa lengo la kuboresha usafirshaji salama wa kemikali. Aidha, tutapata wasaa wa kupata mada itakayotukumbusha majukumu yetu pamoja na mifano halisi ya changamoto ambazo zinajitokeza kuhusiana na usafirishaji salama wa kemikali,”. 

“Ni matumaini yangu kuwa kila mmoja wetu atashiriki kikamilifu katika kuchangia majadiliano kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wa majukumu yetu na kutekeleza ipasavyo kuimarisha utekelezaji wa majukumu yetu na kutekeleza ipasavyo,” alisema Dkt. Mafumiko.

Awali alisema Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na majukumu mengine, ni msimamizi wa utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi na Udhitibi wa msimamizi wa utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi na Udhitibi wa Kanuni zake za mwaka 2020. 

Alisema Sheria hii inadhibiti uingizaji, uzalishaji, usafirishaji, usambazaji, uhifadhi na matumizi mengine yote ya kemikali nchini.

Aidha, alieleza kuwa kama ilivyobainishwa hapo awali, mojawapo la jukumu katika utekelezaji wa Sheria ni kusimamia na kuhakikisha usafirishaji salama wa kemikali hasa zile hatarishi.

Kwamba kwa mujibu wa Sheria hii, kila msafirishaji wa kemikali anapaswa kusajiliwa na Msajili, kumjulisha Msajili taarifa zinazohusu mzigo wa kemikali unaosafirishwa, kuzingatia mahitaji yanayotakiwa wakati wa usafirishaji wa kemikali husika, kuzingatia aina ya gari linalohitajika kwa ajili ya kubeba mzigo wa kemikali husika, na kuwa na kibali cha usafirishaji wa kemikali husika. 

No comments