Breaking News

MHE. BASHUNGWA AZIAGIZA HALMASHAURI ZOTE KUWA MASTER PLAN

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amesema uhitaji wa kuwa na Master Plan kwa sasa ni wa Halmashauri zote na sio zile zenye mradi tu.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo wakati akipokea Taarifa ya Miradi ya Tscp, Ulgsp na Dmdp kutoka kwa kikundi kazi kinachosimamia miradi inayotekelezwa kwa fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia na kusimamiwa na Wakala wa barabara za mijini na vijijini(TARURA).
Amesema katika Taarifa yenu nimesikia kuwa Mpango Kabambe (Master Plan) imeandaliwa kwenye Halmsahuri zilizonifaika na Mradi tu kwenye Miji 18, Majiji na Manispaa pamoja na Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam lakini kwa namna Miji yetu inavyokua kwa kasi Mpango Kabambe inatakiwa kuandaliwa kwenye Halmashauri zote nchini hivyo mjenge hoja kwenye miradi inayokuja ili Halmashauri zilizobakia nazo ziweza kuwa na Master Plan.
Kwa sasa lazima Serikali tuwe mbele ya mipango ya wananchi, tupange miji yetu mapema ili wananchi wakute mpango wa matumizi bora ya Ardhi na kusitokee athari yeyote baadae ya kiuchumi au kisaikolojia kwa wananchi.
Waziri Bashungwa yupo ziarani Jijini Dar es salaam kukagua utekelezaji wa mradi wa Mabasi yaendayo haraka na Miradi inayotekelezwa chini ya fedha za mkopo toka Benki ya Dunia.

No comments